SERIKALI KUENDELEA KUCHUKUA HATUA KWA WAZALISHAJI NA WASAMBAZAJI WA MIFUKO ISIYOKIDHI VIWANGO – WAZIRI ZUNGU

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa wazalishaji na wasambazaji wa mifuko isiyokidhi viwango ili kudhibiti uchafuzi utokanao na mifuko hiyo.
2-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Mussa Azzan Zungu akizungumza kabla ya kushuhudia zoezi la uteketezaji wa shehena ya mifuko isiyokidhi viwango. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Rahabu Solomon, kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kati wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Novatus Mushi
  • Zungu alitoa kauli hiyo Itigi Wilayani Manyoni mkoani Singida leo baada ya kushuhudia zoezi la uteketezaji wa zaidi ya tani 11.53 za mifuko mbadala aina ya non-woven iliyokamatwa katika mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma.
  • Katika zoezi hilo lililofanyika kwa kutumia kichomeo taka cha kisasa cha Hospitali ya Mt. Gaspar iliyopo wilayani humo aliwataka wananchi kutonunua mifuko isiyokidhidhi viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kufanya hivyo watengenezaji hawatapata soko na hivyo itaisha.
M1-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiangalia kichomeo cha kinachotumika kuteketeza mifuko isiyokidhi viwango vya okea sehemu ya mifuko isiyokidhi viwango iliyokamatwa katika mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma na kuteketezwa katika kichomeo cha kisasa katika Hospitali ya Mt. Gaspar iliyopo Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida
  • “Mifuko hii ni michafu na inaharibu mazingira, Serikali imeshatoa agizo na sheria imetungwa lakini mifuko hii inarudi hapa wafanyabiashara wana kiburi wanadharau mamlaka na sisi tutachukua hatua stahiki, lakini tutaendelea kutoa elimiu kwa wananchi” alisisitiza Zungu.
  • Alitoa rai kwa wazalishaji, wasambazaji na wananchi kwa ujumla kuwa ni kosa kisheria kutumia mifuko aina ya non-woven isiyokidhi viwango vya ubora na hatutasita kuchukua hatua kwa mtu yeyote au kiwanda kitakachozalisha mifuko mbadala isiyokidhi viwango vya ubora.
m3-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Mussa Azzan Zungu akitembelea wafanyabiashara na wananchi kuwahamasisha matumizi ya mifuko mbadala inayokidhi viwango katika maeneo ya Halmashauri ya Itigi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
  • Aliongeza kwa kuhamasisha jamii itumie mifuko yenye viwango Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwani watengenezaji wa mifuko hawalipi kodi na inachafua mazingira na pia kutasaidia kuinua viwanda vyetu.
  • Aidha waziri huyo katika ziara hiyo aliyotumia pia kutembelea masoko na maduka na kutoa elimu kuhusu matumizi ya mifuko mbadala alilielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuendelea na ukaguzi wa mifuko isiyokidhi viwango na hatua zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
m4-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Azzan Zungu akihamasisha wafanyabaishara ndogondogo kuhusu matumizi ya mifuko iliyokidhi viwango vya ubora alipokuwa akitembelea masoko na maduka mbalimbali kwenye Halmashauri ya Itigi mkoani Singida baada ya kushuhudia zoezi la uteketezaji wa mifuko isiyokidhi viwango.
  • Awali katika taarifa yake Meneja wa Kanda ya Kati wa NEMC Novatus Mushi alisema katika operesheni hiyo, Baraza likishirikiana na wataalamu kutoka TBS, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa husika (REME), Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya husika, Jeshi la Polisi na idara nyingine za serikali walifanya ukaguzi katika maeneo ya masoko, maduka ya bidhaa za vyakula, na stoo za kusambaza bidhaa mbalimbali.
m6-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Azzan Zungu akishuhudia shehena ya mifuko isiyokidhi viwango tayari kwa kuteketezwa
  • Alisema katika zoezi hilo, jumla ya tani 3.03 za mifuko iliyopigwa marufuku ilikamatwa. Aidha, kufuatia operesheni za awali zilizofanywa na NEMC Juni hadi Mushi alifafanua kuwa Desemba, 2019 kiasi cha tani 8.5 za mifuko iliyopigwa marufuku na ile isiyokidhi viwango ilikamatwa hivyo, kufanya jumla ya kiasi cha mifuko iliyokamatwa kufikia tani 11.53.
  • Zoezi hilo lilishuhudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Solomoni, Kamati ya Ulinzia na Usalama ya Wilaya hiyo na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA AFRIKA MASHARIKI SALAMA KWA MAZINGIRA – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *