- Kiasi cha fedha za kitanzania bilioni 90 zimetolewa na Serikali ya Canada kupitia mradi wa Global Afairs kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa vyuo vya ualimu nchini ikiwemo chuo cha Kabanga ambacho kipo katika hatua za awali.
- Akifungua mkutano wa wadau kitengo cha mafunzo ya elimu yanayolenga utoaji wa mafunzo kwa walimu wa vyuo vya ualimu nchini Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu,sayansi na teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo amesema fedha hizo zitawezesha ujenzi wa vyuo vipya na vingine kuongezewa miundombinu ili viweze kutoa mafunzo kwa ufasaha.
- Ameongeza kuwa ujenzi wa chuo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi wa sita mwaka huu ambapo ameishukuru serikali ya Canada kupitia mradi huo kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana kwani tayari wameanza kuona matokeo kupitia kwa wakufunzi na walimu waliopatiwa mafunzo hayo na kuongeza uwezo wao.
- Vilevile amesisitiza kwa kuwataka walimu ambao hupatiwa mafunzo mbalimbali yahusuyo kutumia fursa hiyo kama sehemu ya kuongeza uelewa na ufanisi katika utendaji kazi wao ili kuweza kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya elimu nchini.
- Amesema Lengo la Mradi huo ni kuimarisha ufundishaji katika vyuo vya ualimu nchini ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezo wa vyuo katika kufundisha kwa kutoa mafunzo kazini kwa walimu sambamba na upelekaji wa vifaa vya kusaidia ufundishaji katika vyuo nchini.
- Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu kutoka katika Wizara ya elimu,sanyansi na teknolojia idara ya sera na mipango Ignas Chonya amesema kuwa mradi huo niwa miaka mitano na unajielekeza kwenye mambo yote yanayogusa elimu ya ualimu,miundombinu,vitendea kazi pamoja na kuwajengea uwezo wa kitaaluma wafanyakazi.
- Ameeleza kuwa mradi huo pia kuendeleza somo la hisabati nchini ili kutatua changamoto hiyo ambapo wameweza kuzifikia shule za msingi na sekondari katika halmashauri 20 nchini ambazo zimekuwa na ufaulu hafifu kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa jwa mujibu wa takwimu wa baraza la mitihani la taifa na tayari wameshapata matokeo chana katika halmashauri 12 walizoanza nazo.
- Ameongeza kuwa kufuatia hatua hiyo waliyoianza ambayo imewapatia mafanikio,mwaka huu wameongeza wigo na kuzifikia halmashauri 20 ambapo wataendelea kufanya hivyo kwa kuziliea mpaka zitakapovuka kwenda kwenye ufaulu wa kuridhisha.
- Pamoja na hayo amesema kuwa mradi huo umejielekeza kuwajengea uwezo wakufunzi wote kwa kutumia tehama kama nyezo ya ufundishaji na ujifunzaji ambapo wameweza kuvifikia wakufunzi wa vyuo vyote vya serikali 35. Na Jusline Marco – Arusha
Ad