RC SHIGELLA ATEMBELEA KIWANDA KIPYA CHA KUZALISHA KADI ZA KIELEKTRONIKI

Serikali imetakiwa kuweka utaratibu utakaowezesha taasisi za Umma na watu binafsi, kuacha kuagiza kadi za kielektroniki nje ya nchi na badala yake watumie zinazozalishwa nchini ili kujenga uchumi wa viwanda.

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella, alitoa pendekezo hilo wakati alipotembea kiwanda kipya cha kuzalisha vocha na kadi mbalimbali kinachojulikana kwa jina Rushabh Investment Ltd kilichopo Jijini Tanga.

Alisema akiwa kiongozi wa mkoa huo, atashawishi Serikali kuweka utaratibu wa bidhaa hizo za Kieletroniki zitakazozalishwa kiwandani hapo, zitumike katika sekta mbalimbali hapa nchini.

Shigella alikunwa zaidi hasa baada ya kuelezwa kwamba kiwanda hicho pindi kitakapoanza kazi rasmi, kitakuwa cha pili barani Afrika. Kiwanda kingine kama hicho kipo Afrika Kusini.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella, akikagua mitambo ya kiwanda kipya cha kuzalisha kadi za Kieletroniki kilichopo Jijini Tanga. Wa kwanza mwenye Kanzu ni Rashid Ahmed Liemba na anayefuata ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daud Mayeji.


“Niombe kwa serikali mara baada ya kiwanda hiki kuanza uzalishaji basi tuachane na uagizaji wa kadi kutoka nje ya nchini kwani sasa huduma hiyo ipo humu nchini, na kwamba itasaidia kujenga uchumi wa nchi, ” alisema Shigella.

Mwekezaji wa kiwanda hicho cha Rushabh Investment ltd Rashid Ahmed ‘maarufu kwa jina la Liemba’ alisema uwepo wa kiwanda hicho licha ya kutoa ajira kwa vijana hapa nchini lakini pia kitakuwa ni ukomboozi kwa nchi za Afrika.

Alisema kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa za kadi hasa katika nchi za Afrika kutokana na kukua kwa teklonojia lakini pia nchi nyingi zinalazimika kuagiza na kutengeneza bidhaa hizo nje ya nchi.

Hata hivyo, Liemba ambaye ana kiwanda kingine cha kuzalisha Chokaa ya kisasa kabisa cha Nelkant, alisema awali walikuwa wakizalisha kadi za simu pekee lakini sasa wamekiongezea uwezo zaidi.

Alisema wamekiendeleza ili kiweze kuzalisha kadi zote za Kieletroniki zikiwemo kadi za benki, Bima ya afya, kadi ya mpiga kura na kadi nyingine zote, lakini hakijaanza kazi baada ya wataalamu wake watakaoendelea na ufungaji wa mashine kukwama nchini Ujerumani kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

“Kiwanda hiki kilikuwa kianze kazi kabla ya mwezi wa nne lakini wataalamu wa mitambo wako Ujerumanj hivyo wameshindwa kuja kufunga mitambo kutokana na ugonjwa wa Corona.

Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *