WAZIRI MKUU AKAGUA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA JNHPP

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115 na amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka asimamie mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nishati Dkt. Medad Kalemani, wakati alipokagua hatua za utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, May 14, 2020


Vilevile, Waziri Mkuu amemwagiza mkandarasi anayejenga mradi huo aukamilishe kwa wakati kwa sababu imebainika kuwa mvua zinazoendelea kunyesha nchini haziathiri utekelezaji wa ujenzi huo.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Alhamisi Mei 14, 2020) akiwa katika ziara ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi huo. Amesema ameridhishwa maedeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa kimkakati.

Ad
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nishati Dkt. Medad Kalemani, wakati alipokagua hatua za utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, May 14, 2020


“Nimetembelea eneo la mradi na kujionea shughuli zote zinazoendelea, kazi inayofanyika ni ya uhakika huku kukiwa na matumaini makubwa ya kukamilisha mradi mapema kabla ya muda uliopangwa.”

Mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji unajengwa na kampuni ya Arab Construction kwa pamoja na kampuni ya Elsewedy Electric zote za kutoka nchini Misri. Mradi huo unatarajiwa kuzalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye grid ya Taifa na kuifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Kaimu Mhandisi Mkazi, Injinia Lutengano Mwandambo, wakati akikagua hatua za utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, unaojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi, May 14, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Mbali na kuliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, pia mradi huo umewezesha kupungua kwa changamoto ya ajira baada ya Watanzania wengi wakiwemo wakandarasi kupata ajira za kudumu na za muda mfupi.

Kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo, kutaiwezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kitakachosaidia kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa uchumi wa viwanda na mradi wa reli ya kisasa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, (watatu kushoto) akikagua hatua za utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2,115, unaojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi, May 14, 2020.


Hafla ya utiaji saini ya Mkataba wa Ujenzi wa Mradi ilifanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Desemba, 2018 na kushuhudiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mostafa Madbouly. Mradi huu ni njia sahihi ya kufikia Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *