KIPAUMBELE CHA SERIKALI NI KUWALIPA WASTAAFU MAFAO YAO – WAZIRI MPANGO

Waziri wa fedha na mipango Dkt Philip Mpango

Serikali imesema moja ya kipaumbele chake ni kuhakikisha wazee wanastaafu kwa amani kwa kuwalipa mafao yao kadri inavyostahili.

Waziri wa fedha na mipango dkt Philip Mpango amesema hayo mei 15 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu mchango wa mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu.

Ad

Akichangia mjadala wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2020/2021 Mtaturu ameiomba wizara kushughulikia mafao ya wastaafu ambao wamekuwa wakicheleweshewa kupatiwa mafao yao pindi wanapostaafu.

“Kuna baadhi ya Wastaafu wetu wanastaafu lakini wanashindwa kulipwa kwa wakati na wengi wao wamelitumikia Taifa hili kwa uadilifu mkubwa,niwaombe Wizara ya Fedha tuwe tunawalipa kwa wakati.

Ametolea mfano katika wilaya ya Ikungi, “Kuna wazee wawili Mohammed Ntandu na Gamiliel Massawe wanalalamika hawajatendewa haki yao mpaka sasa hivi miezi saba,wakienda kwa wenzetu NSSF hawawapi majibu mazuri naomba mh waziri kuwe na connection nzuri kati ya mikoa na hazina ili kuwasaidia wastaafu wapate mafao yao mapema,”alisema Mtaturu.

Amesema kwa sasa serikali wanajitahidi kadri inavyowezekana kuhakikisha wazee wanaostahili mafao wanayapata kwa wakati.

“Nimepokea kilichosemwa na mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,na bahati nzuri ameniwasilishia document hivyo nitazifuatilia,kinachotusumbua mara nyingi ni udhaifu katika taarifa lakini wizarani tumeweka kipaumbele chetu ambacho ni kuhakikisha wazee wetu wanastaafu kwa amani kabisa,”alisema Dkt Mpango.

Katika mchango wake Mtaturu amewaomba watanzania kuhakikisha katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu wanachagua CCM chama ambacho ndicho kitakachowaletea maendeleo.

“Unapokuwa na aina ya vyama vya siasa ni lazima uwe na vyama vyenye focus ya kuwatumikia wananchi,na mnaona wenyewe watanzania wameona vyama hivi kuna baadhi ya vyama tukikutana octoba kitatoka kuwa chama cha siasa kitakuwa ni kikudi cha watu wawili watatu.

“Nimtie moyo Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kwa hakika watanzania wamemuelewa watanzania hawatamuacha haya yote makubwa aliyoyafanya hayatafutika katika uso wa watanzania,nimtakie kila la kheri,sisi wapiganaji tupo pamoja nay eye na kwa Singida Mashariki nimuhakikishie kura nyingi,mbunge nipo na madiwani wote watapatikana na CCM,”alisisitiza Mtaturu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Nani aliyeunda Jumuiya ya Madola na kwa nini?”

Malkia Elizabeth II pamoja na mawaziri wake wakuu wa Jumuiya ya Madola mwaka 1962. Picha: …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *