TUMEKUBALIANA NA RAIS KENYATTA MAWAZIRI WETU WA UCHUKUZI NA WAKUU WA MIKOA KUKUTANA KUMALIZA TATIZO LA MIPAKANI – RAIS MAGUFULI

Rais Dkt John Magufuli amesema kuwa Viongozi wa Mikoa wasitatue matatizo kwa jazba, na badala yake amewataka viongozi hao kukutana na kutatua changamoto iliyopo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nzega mkoani Tabora (hawaonekani pichani) wakati akielekea mkoani Singida.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Singida aliposimama kuwasalimia akitokea Chato Mkoani Geita, Aidha amewaangiza Viongozi wa mikoa inayopakana na Kenya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutatua changamoto hiyo.

Ad

“Niliongea na Rais Kenyatta na hata leo nimeongea naye, kuna migogoro kule mipakani tumekubaliana na Rais Kenyatta kwamba Waziri wa Uchukuzi wa Kenya na Tanzania, wakuu wa mikoa ya mipakani wakutane na wenzao wa Kenya ili kujadili na kumaliza tatizo hilo” – Rais Dkt

Rais Magufuli amewaomba Viongozi wa mikoa ya Tanzania inayopakana na kenya kutanguliza Utanzania na Ukenya kwa kuzingatia uchumi wa nchi hizo kwani wafanyabiashara wa Kenya wanahitaji kufanya biashara Tanzania na Watanzania wanahitaji kufanya biashara Kenya

“Nimeambiwa kuna magari kule ya Wakenya yamekwamishwa haiwezekani tukawa kwamisha wanakuja kufanya biashara, lakini pia magari ya Tanzania hayawezi yakakamishwa kwenda Kenya” Rais Magufuli

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *