MANYANYA AAGIZA BIDHAA ZA SAMAKI ZOTE ZINAZIUZWA NJE YA NCHI KUWEKEWA ALAMA AU MAELEZO KUONESHA KUWA NI BIDHAA KUTOKA TANZANIA

Na Eliud Rwechungura Wizara ya Viwanda na Biashara

Ikiwa ni siku moja baada ya Ndege ya Ethiopia Airlines kuanza kufanya safari zake katika mkoa wa Mwanza kwa ajiri ya kubeba minofu ya  samaki inayovuliwa katika ziwa victoria na kuchakatwa na viwanda vilivyopo mkoa wa Mwanza, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella Manyanya ametembelea kiwanda cha Tanzania Fish Processors Ltd kinachojihususha na kuchakata samaki kilichopo mkoa wa Mwanza.

Ad

Ziara ya Mhandisi Stella Manyanya ilikuwa na lengo la kujione uzaliahaji unaofanywa na viwanda  vya samaki pia kujua changamoto wanazozipitia katika hatua za kuchakata samaki ambao watakuwa wanasafirishwa na ndege ya Ethiopia Airline kwenda katika nchi mbalimbali.

Baada ya kujionea shughuli nzima ya uchakataji wa samaki Mhe. Stella manyanya ameelekeza viwanda vyote nchi vya samaki nchini vinavyosafirisha minofu ya samaki kwenda nje ya nchi kuhakikisha vifungashio vyote vinawekewa alama au maelezo ya kuonesha  bidhaa hizo zinatoka Tanzania (Made in Tanzania)  kabla ya kutoka nje ya Viwanda au kwenye mipaka ya Tanzania.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella Manyanya{kushoto} akiwa ameshikilia samaki wanaovuliwa katika ziwa Victoria kwa ajili ya kuchakwatwa na kiwanda Tanzania Fish Processors Ltd kilichopo mwanza kwa ajiri ya kusafirishwa na kuuzwa katika nchi mbalimbali. Tarehe 22 mei 2020

Akitoa taarifa Mkurugenzi wa rasilimali watu wa kiwanda cha Tanzania Fish Processors Ltd Bw. Goodfray Samwel amemushukuru Rais Magufuli kwa kuwa na maono ya kufanya Tanzania kuwa ya nchi yenye uchumi wa viwanda pia akampongeza kwa kuendelea kuweka sera nzuri Zenye malengo ya kuendeleza viwanda pia kufufua viwanda vingine ambavyo vilikuwa havifanyi kazi.

Aidha, Bw. Goodfray ameeleza baadhi ya changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo  ambazo ni Uvuvi haramu ambao hupunguza sehemu bora za mazalio ya Samaki,  Uwepo vyumba vidogo vya kutunzia samaki kataka viwanja vya ndege (cold rooms), Mchanganyiko wa uvuvi usio endelevu na uchafuzi wa mazingira ambavyo husababisha kiasi cha samaki na kipato kupungua pia akaeleza changamoto ya wanunuzi wa soko la ulaya kupungua ambao wanataka minofu mikubwa, sambamba ya hayo akaeleza changamoto ya usafiri ambayo imeanza kutatuliwa na serikali kwa kuruhusu ndege ya Ethiopia Airlines kutua Mwaza kwa ajiri ya kubeba samaki.

Wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata samaki cha Tanzania Fish Processors Ltd wakiendelea na kazi ya uchakataji wa samakiwanaosafirishwa na kuuzwa katika nchi mbalimbali. Tarehe 22 mei 2020

Nae Naibu waziri Wa Viwanda na Biashara ametoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano ili kuboresha viwanda vyote nchini hasa viwanda vya samaki ambazo zina soko kubwa katika nchi mbalimbali kote duniani.

“Serikali imejipanga kuhakikisha inaboresha sekta ya uvuvi ambayo ni sekta muhimu katika kukuza uchumi  kutoka na umuhimu wake wa uhitaji wa malighafi ya samaki ambazo zinasaidia viwanda vya samaki kote nchini kuendelea kufanya kazi na kukua kwa kasi, kutoka na changamoto nilizozisikia Serikali imejipanga kuanzisha taasisi mbalimbali za utafiti wa samaki katika ziwa victoria, pia tumejipanga kuanzisha masoko ya samaki yakiwa na lengo la kuchochea sekta hii, sambamba na hayo Tutakuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara kati ya serikali na vyama vya wafanyabiashara wa samaki ambayo itasaidia kutatua kero mbalimbali ambazo wafanyabiashara wanakabiriana nazo’’

Ad

Unaweza kuangalia pia

Benki ya NMB Tanzania yapongezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

kwakuwa Kinara katika utendaji wake, kutengeneza faida kubwa ya mfano wa kuigwa na mashirika na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *