Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya amefanya ziara June 3 akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Hamza Johari na kuisisitiza mradi huo kufanya kazi usiku na mchana ili uweze kukabidhiwa ifikapo Septemba 26 mwaka huu.
Aidha, amewataka wasimamizi wa mradi huo ambao ni Tanroads kusimamia kwa ukaribu ili mradi ukamilike kwa wakati na uanze kuwanufaisha Wananchi wa Mtwara na maeneo Jirani.
Ujenzi huo wa mradi wa ukarabati na Upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mtwara upo chini ya Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group Company Limited ya China kwa gharama ya shilingi billion 50, 366,063,531.38. Na Mtwara Online Tv