NAIBU WAZIRI UJENZI AAGIZA KIPANDE CHA BARABARA NJOMBE -MORONGA KIKAMILISHWE IFIKAPO MWEZI OCTOBA MWAKA HUU

Na Amiri kilagalila,Njombe

Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi  Elias kwandikwa amemuagiza mkandarasi anayejenga barabara ya Njombe kuelekea wilayani Makete kipande cha Njombe-Moronga kuhakikisha anakamilisha ujenzi  wa kipande hicho na kuhakikisha imekamilika ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

Agizo hilo amelitoa wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo amesema anataka kuona ujenzi huo unakamilika ili wananchi waendelee kunufaika na barabara hiyo kwa kuwa serikali imeshawalipa fedha makandarasi wote nchini.

“Mkandarasi afanye kazi kadri itakavyowezekana barabara hii kipande hiki ifikapo mwezi Octoba iwe imekamilika nafikiri hakuna mashaka kwasababu kazi imefanyika.

Na sisi kama serikali tumejipanga vizuri kuendelea kuwalipa wakandarasi ili tuhakikishe watanzania wanafurahi matunda ya koi zao”alisema Kwandikwa Meneja wa Tanroad mkoa wa Njombe mhandisi Yusuph Mazana amesema tayari mkandarasi huyo ameshalipwa fedha zote na kazi zimekuwa zikienda vizuri licha ya mkoa wa Njombe kuwa na vipindi virefu vya mvua huku mhandisi mshauri  wa barabara hiyo Lusekelo Kijalo kwa niaba ya mkandarasi wa barabara hiyo amesema ni lazima wakamilishe ujenzi huo kama mkataba unavyoelekeza.

Christopher Ole Sendeka ni mkuu wa mkoa wa Njombe ambaye amesema endapo barabara hiyo itakamilika hadi kuungana na mkoa wa Mbeya itawasaidia sana wakulima kusafirisha mazao yao kwenda katika uwanja wa ndege wa Songwe.

“Tanzania tunaweza ndio maana Mh.Rais amethibitisha kwa vitendo kujenga barabara hii itakayokuwa na km 107 kwa kiwango cha lami kutoka Njombe – Moronga na sehemu ya pili kutoka Moronga kwenda Makete.Lakini nia ni kuendeleza barabara kutoka Iwawa makao makuu ya wilaya ya Makete kwenda Isyonje mkoa wa Mbeya ambayo itawezesha wananchi wa mkoa wa Njombe kusafirisha mazao yao ya kilimo kupitia uwanja wetu wa Ndege wa Songwe”alisema Ole Sendeka.

Unaweza kuangalia pia

KWA MARA YA KWANZA WATAALAMU WAZAWA WAZIBUA MISHIPA PACHA YA MOYO ILIYOZIBA KWA ASILIMIA 95

Kwa mara ya kwanza wataalamu wazawa wa magonjwa ya moyo na wazibuaji wa mishipa ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.