WIZARA YA MAJI KUFANYA UTAFITI NA USANIFU WA MRADI MKUBWA MAJI KUTOKA ZIWA VICKTORIA KUPELEKA JIJINI DODOMA

Wizara ya Maji inatarajia kufanya utafiti mkubwa na usanifu wa mradi mkubwa wa maji wa kuchukua maji kutoka ziwa vicktoria kupeleka Mkoani Dodoma kwa kupitia Mkoani Singida katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.Kitila Mkumbo alitoa kauli hiyo kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17, Singida ikiwa ni moja ya mikoa hiyo.

Ad

Aidha Katibu Mkuu huyo wa maji alisisitiza kwamba kwa kuwa fedha za mradi huo zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha,hivyo anaamini katika kipindi cha miaka mitano ijayo mikoa ya Singida na Dodoma inaweza ikapata maji kutoka ziwa Viktoria.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *