SERIKALI IMEFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KWENYE SEKTA YA AFYA HUSUSANI KATIKA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIBINGWA – NAIBU WAZIRI MOLLEL

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel ametembelea na kukagua hali ya utaoaji wa huduma katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI pamoja na kuzumza na watumishi ili kufahamu changamaoto mbalimbali wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku.

Akizungumza na viongozi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam Dkt. Mollel alisema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya hususani katika kuimarisha huduma za kibingwa hapa nchini.

Ad

“Kuwepo kwa uwekezaji huu kumewafanya wataalamu wa Taasisi ya MOI kuokoa maisha ya watanzania wengi ambao wametibiwa hapa nchini pia imeokoa zaidi ya bilioni 38.4 ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa hao kufuata huduma za kibingwa nje ya nchi. Haya ni mafanikio makubwa ambayo lazima watanzania wafahamu kwamba Serikali hii inawajali wananchi wake,” alisema Dkt. Mollel.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface alisema katika Uongozi wa Serikali ya awamu ya tano Taasisi hiyo ilipokea bilioni 16.5 kutoka Serikalini fedha ambazo zilitumika kukamilisha mradi wa ujenzi wa awamu ya tatu ya MOI pamoja na kununua vifaa tiba vya kisasa ambavyo vimesaidia kupatikana kwa huduma nyingi za kibingwa na hivyo kumaliza rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi.

“Tumeanzisha huduma nyingi za kibingwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwenye Taasisi yetu, wiki iliyopita Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alizindua kituo cha kitaifa cha teleradiolojia kilichopo hapa MOI na wiki chache zijazo tutaanza majaribio ya mitambo ya maabara ya upasuaji wa Ubongo,” alisema Dkt. Boniface.

Dkt. Boniface alisema huduma ya maabara ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu itaanza kutolewa hapa nchini wiki chache zijazo na hivyo kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika zinazotoa huduma hiyo.

“Uwepo wa Maabara hii utatupa heshima kama nchi kwani katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati hakuna maabara yenye vifaa vya kisasa kama hivi ambavyo Serikali ya awamu ya tano imevinunua na kusimikwa hapa MOI, kwa hili tunamshukuru Rais 

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *