UJENZI WA BARABARA YA TABORA – KOGA – MPANDA KM 324.7 KWA KIWANGO CHA LAMI WAFIKIA ASIMILIA 48


Kazi za ujenzi wa tabaka la juu la lami ukiendelea katika barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 342.7); sehemu ya Usesula – Komanga, mkoani Tabora.
Kazi za kusambaza lami katika sehemu ya barabara ya Komanga – Kasinde ikiendelea. Kazi hiyo inafanywa na mtambo maalum wa kisasa unaogusa upana wote wa barabara na wenye uwezo wa kusambaza lami kilometa 1.2 kwa siku.
Mtambo wa kushindilia lami ukiendelea na kazi katika barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 324.7); sehemu ya Kasinde – Mpanda, mkoani Katavi. Ujenzi wa sehemu hiyo umefikia asilimia 48.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kassanda, wakitoka kukagua ujenzi wa Daraja la Koga (m 120) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 60 wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Katavi, Mhandisi Martin Mwakabende, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, hatua ya ujenzi wa Daraja la Koga (m 120), ambalo mpaka sasa umefikia asilimia 60.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rachel Kassanda, wakati akikagua ujenzi wa sehemu ya barabara ya Komanga – Kasinde (km 112.18), inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Katavi.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya China Wu Yi kukamilisha ujenzi wa Daraja la Mto Koga lenye urefu wa mita 120 ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu na kuruhusu magari kupita juu yake badala ya kutumia daraja la zamani.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kukamilika mapema kwa ujenzi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 342.7), kwa kiwango cha lami kwani itaongeza uchumi wa wananchi na kuongezeka kwa shughuli za kibiashara kwa kuwa ni mikoa yenye uzalishaji mwingi wa bidhaa za kilimo.

Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

USHAWISHI WA TANZANIA DUNIANI UTATEGEMEA NA UBORA WA SERA YA MAMBO YA NJE INAYOREKEBISHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu-Zanzibar, Mhe.  Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya ufunguzi ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.