TAASISI YA BENJAMINI MKAPA (BMF) YAAJIRI WATU 575

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru akizungumza na na baadhi wataalamu wa afya waliopata ajira ya muda kupitia taasisi ya Benjamin Mkapa

Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF) kupitia ufadhili wa mashirika ya Maendeleo ya Irish Aid, UKAID-DFID na UNFPA, imeajiri watumishi wa  kada mbalimbali za afya 575 kwa muda wa miezi sita kuanzia mwezi Julai 2020 wtakaofanya kazi katika Halmashauri 72 zilizopo kwenye mikoa mitatu.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ajira hizo Julai 8,2020 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchemba amewaasa wote watakaoajiriwa kupitia mradi huo wa BMF  kufanya kazi kwa kufuata taratibu za kitaalamu huku Pia akiwasishi kuzingatia maadili ya utumishi na kujitahidi kuwa mfano katika maeneo watakayokuwa wakifanya kazi. 

“Uadilifu wenu katika utoaji wa huduma ni wa muhimu kwani mtakuwa ni kioo cha namna sekta yetu ya Afya inavyofanya kazi”, amesema Prof. Mchembe.Amesema, ajira hizo wanazoingia na Taasisi ya BMF ni ajira za muda wa miezi sita.

Ad

“Mmepangwa kufanya kazi katika maeneo yaliyopewa kipaumbele chini ya mikoa 13 iliyopo hapa Tanzania bara. Maeneo mliyopangwa ni yale ambayo Serikali imeona ni vyema kuongeza nguvu katika kuimarisha huduma za Kinga na Tiba dhidi ya maradhi mbali mbali mfano UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu, Magonjwa ya Mlipuko mfano Corona n.k pamoja na kuimarisha huduma ya Afya ya Uzazi… wote mliochaguliwa mmepewa kipaumbele hicho kwa kuwa mlikuwa mnajitolea katika maeneo mliyopangwa hivyo basi, Serikali ikaona ni vyema kuwatumia katika mfumo rasmi kwa kipindi cha miezi sita”, amesema Prof. Mchembe

Katibu Mkuu akiwa kwenye picha ya pamoja na menejiment ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Benjamin Mkapa pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya

Jumla ya Halmashauri 72 zilizopo katika mikoa 13 imepewa kipaumbele ikiwemo Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Tanga, Mara, Pwani, Dodoma, Arusha, Mtwara, Kigoma, Mwanza, Simiyu, Mbeya na Songwe.

Mbali na mikoa hiyo 13 ya Tanzania bara, pia mradi utawezesha upangaji wa watumishi 21 kwa upande wa Tanzania Visiwani ambapo huo mchakato wake unaendelea ili kuweza kuzingatia taratibu za ajira za Tanzania Visiwani.

Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Dkt. Ellen Senkoro  amesema kuwa Tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Mkapa takriban miaka 14 iliyopita, taasisi imeendelea kushirikiana na serikali, katika jitihada zake za kuhakikisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwemo pia kupatia ufumbuzi wa kupunguza upungufu wa wataalamu wa afya, ambao mpaka sasa umekadiriwa kuwa ni wa asilimia 52 ya watumishi wote wanaohitajika hapa nchini.

Amesema, watumishi hao 575 wanatoka katika fani 13 ambazo ni Mteknolojia Maabara  Mteknolojia Maabara Msaidizi, Tabibu ,Tabibu Msaidizi, Daktari II, Afisa Muuguzi Msaidizi, Afisa Muuguzi  Afisa Ustawi wa Jamii , Afisa Ustawi wa Jamii Msaidizi , Mteknolojia Dawa , Mteknolojia Maabara Msaidizi , Afisa Afya Mazingira, na  Afisa Afya Mazingira Msaidizi.

Aidha Dkt, Senkoro ameshukuru Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI kwa ushirikiano wao madhubuti na mkubwa sana walioutoa katika kufanikisha ajira hizo. 

Naye, Katibu Mkuu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema, Muhimbili inayo furaha kufanya kazi na Taasisi ya BMF ana kwamba watumishi 575 watakaopata ajira hizo, watumishi 80 wamepangiwa kufanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *