RAI YANGU KWA WANANCHI WATANZANIA TUUNGANE TUWE KITU KIMOJA – WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZEGO PINDA

Alichozungumza Waziri Mkuu Mstaafu Mizego Pinda akiwa Ikulu Chamwino jijini Dodoma, Julai 12, 2020

“Mhe Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, Waheshimiwa Viongozi wote wa meza kuu, Mhe. Rais nimepewa nafasi hii kwanza nishukuru sidhani kama nilistahili lakini niseme mambo mawili”

Ad

“jambo la kwanza Mhe. Rais naomba niseme kwa dhati nikupongeze wewe na watanzania kwa ujumla kutokana na taarifa ile ya benki ya Dunia kwamba Tanzania sasa imetambulika kuingi katika uchumi wa kati si jambo dogo nimeona kwenye mitandao baadhi ya Watanzania wanabeza na mimi nikasema nadhani ni wagonjwa akili.”

“Kwasababu kama unavyojua ni kwamba tumetoka katika ile hatua ambayo tulikuwa tunatazamwa kama moja ya nchi maskini Duniani jitihada zilizofanyika ndani ya miaka mitano ndio zimetupa hiyo heshima unastahili pongezi wewe na timu yako lakini na wananchi wote wa Tanzania hapo katika hili tupo pamoja.”

“Rai yangu kwa wa Tanzania tumeingia katika uchumi wa kati lakini kazi iliyo mbele yetu ni kubwa sana kwa sababu watanzania wengi pamoja na hatua hiyo tuliyofika tuko kwenye ile ngazi ya chini kabisa katika mchakato mzima wakiwa nchi ambayo inasemekana kuwa sasa ni ya uchumi wa kati kwahiyo tuna hatua karibu nne ambazo lazima tuziangalie kwa makini”

“Na mimi naendelea kuomba serikali yako ukishaitengeneza baada ya uchaguzi mkuu jambo hili tungelipa nafasi kubwa ili watanzania wote tuelimike nini kinachotakiwa kila Mtanzania ili sasa tutoke kwenye ngazi ile ya chini tuingie ngazi ya chini kati, tupande hadi wastani dola 4000 takriba karibu shilingi milioni 10 hivi kwahiyo safari bado ni ndefu na mimi namshukuru Mungu kwamba tumefikia hatua hii kipindi chako na hii inaonyesha kazi nzuri uliyoifanya”

“Jambo la pili kwa watanzania naomba nitumie pia nafasi hii kukupongeza wewe serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa hatua kubwa tukiyoifikia hivi juzi kumpata mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ndugu yetu Hussein Ali Mwinyi sisi tunaomjua comrade huyu hatuna shaka naye hata kidogo, ni muadilfu ni mtu ambaye ataitendea haki Zanzibar”

“Rai yangu kwa wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla tuungane tuwe kitu kimoja ili Zanzibar iweze kupiga hatua ambayo Tanzania kwa ujumla tunatamani tuifikie tukimuunga mkono kijana huyu naamini kabisa Zanzibar itafanya vizuri sana nimeona dalili za mwanzo nzuri na bahati nzuri we mwenyewe umelieleza juzi sitaki kuyarudia nitaharibu uhondo bure”

“Tuna kila sababu kwa Wazanzibar kufanya vizuri katika uchaguzi ujao kuliko miaka iliyopita hasa kazi kwetu Watanzania kazi kwetu Wazanzibar ili tuweze kuipaisha Tanzania ndani yake Zanzibar ikiwa kiungo muhimu sana katika Muungano wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” – Waziri Mkuu Mstaafu, Mizego Peter Pinda

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA SULUHU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA NCHI, WIZARA YA MAMBO YA NJE YA SHIRIKISHO LA JAMHURI YA UJERUMANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na kuagana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.