BALOZI SOKOINE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNDP

Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ukiongozwa na Bi. Christine Musisi – Mwakilishi Mkazi mara baada ya kukamilika kwa kikao cha mashirikiano baina yao. Wengine katika picha ni wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na UNDP
Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (kulia) akiwa katika kikao pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ukiongozwa na Bi. Christine Musisi ambae ni Mwakilishi Mkazi. Kikao hicho kimelenga kuimarisha ushirikiano katika hifadhi ya Mazingira hususan katika maeneo ya Mabadiliko ya Tabianchi, Uchumi wa Bahari, Nishati endelevu, Hifadhi ya Bioanuai na Ikolojia. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba – Dodoma.
Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akiagana na Bi. Christine Musisi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada ya kukamilika kwa mkutano baina yao uliojadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mazingira. Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba – Dodoma.
Ad

Unaweza kuangalia pia

USHAWISHI WA TANZANIA DUNIANI UTATEGEMEA NA UBORA WA SERA YA MAMBO YA NJE INAYOREKEBISHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu-Zanzibar, Mhe.  Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya ufunguzi ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.