Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaomba wananchi kutumia redio kutoa maoni yenye tija kwa ajili ya kusaidia Serikali ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Makamu wa Rais amesema hayo katika uzinduzi wa Redio Jamii ya Kati FM mradi wa Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari unaolenga kudhibiti ukatili kwa wanawake na wasichana mjini Zanzibar
Ad
“Naomba nitoe rai kwa UNESCO na waendeshaji wa redio jamii tutakayoizindua na nyingine zote zilizotangulia kuhakikisha kuwa miiko ya kazi ya utangazaji inafuatwa ili kutunza na kuimarisha amani na utulivu wa nchi yetu.
Ni vyema pia mawazo ya makundi yote kwenye jamii ikiwemo wanawake na watu wenye mahitaji maalum yakazingatiwa ili kuhakikisha kuwa redio hii inanufaisha kila mtu katika jamii'” Amesema Makamu wa Rais
Aidha Makamu wa Rais ameagiza kuwa redio zisitumike katika kugawa wananchi bali iwe chachu ya kutoa elimu na kuibua fursa mbali mbali za maendeleo.