WAZIRI ZUNGU ATAKA KUSIMAMIWA VIZURI KWA TAFITI ZINAZOFANYIKA KUHUSU BIOTEKNOLOJIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mussa Azzan Zungu ameelekeza kusimamiwa vizuri kwa tafiti zinazofanyika kuhusu bioteknolojia na kuishauri Serikali kuhusu matumizi yake salama.

Zungu ametoa maelekezo hayo hilo leo Agosti 12, 2020 wakati akizindua Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa jijini Dodoma.

Ad

Alisema kaatika kuhakikisha kunakuwa na usalama na faida ya matumizi hayo kamati hiyo ina jukumu la kupitia maombi ya matumizi ya viumbe na bidhaa zitokanazo na biotejinolojia ya kisasa na kushauri kuhusu sera, sheria, tafiti.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mussa Azzan Zungu akisoma hotuba ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa jijini Dodoma Agosti 12, 2020. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo na Kaimu Mkurugenzi Idara Mazingira, Faraja Ngerageza.

“Chakula na maji vikikosekana taifa litaangamia hivyo naamini kamati hii itasimamia tafiti zake na kutoa ushauri kwa Serikali maana tunaona tafiti nyingi zikifanywa hazifanyiwi kazi zinawekwa chini ya meza,” .

“Kwa awamu hii ya tano mabadiliko yanaonekana Rais Dkt. John Magufuli kwa uzalendo wake na mapenzi yake kwa taifa letu linasonga mbele kwa taifiti na maoni, mapendezo mtaipa serikali,” alisema.

Aidha Waziri Zungu aliongeza kuwa Serikali imeandaa na kuweka nyenzo mbalimbali za usimamizi wa teknolojia hii ikiwa ni pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, Mfumo wa Kitaifa wa  Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa yam waka 2007, Kanuni  za Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa ya mwaka 2009 na miongozo mbalimbali ya mwaka 2010.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa jijini Dodoma Agosti 12, 2020.

Alifafanua kuwa hadi sasa mfumo wa usimamizi umewezesha kufanyika kwa utafiti ndani ya maabara wa mihogo unaolenga kupata ukinzani dhdi ya magonjwa ya virusi vya zao la muhogo, utafiti nje ya maabara wa mahindi yanayovumilia ukame na bungua, kusafirisha chakula cha msaada kupitia bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani.

Pamoja na hayo alisema baada ya kikao cha kwanza cha kamati hiyo ni vyema ikaandaa mpango kazi wa utekelezaji wa majukumu yake katika kipindi cha miaka mitatu kuonesha namna itakavyosaidia kuhakikisha Tanzania inafaidika na matumizi ya teknolojia hiyo.

Awali Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo alisema kuwa kamati hiyo iliyozinduliwa ina jukumu la kusaidia nchi kuhusu matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa.

Mhandisi Malongo alisema kuwa kutokana na sifa walizonazo wajumbe wa kamati hiyo kutoka sekta mbalimbali anaamini watafanya kazi ya kuishauri vizuri Serikali.

“Tuna changamoto kubwa sana tunategemea kamati hii mpya mtuchukue to the next level, nakumbuka tulipata kazi kubwa ya kuelimisha wananchi kuhusu teknolojia hii name nina imani na ninyi,” alisema.

Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia ya Kilimo (OFAB) kwa kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais inaimarisha usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa nchini hususan kwa utoaji wa mafunzo mbalimbali kwa jamii na wataalam wetu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *