WASOMI WAHIMIZWA KUWA WABINIFU

Na Mwandishi Wetu Lushoto Tanga

Wasomi nchini wamehimizwa kutumia rasilimali zinazowazunguka kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni njia mojawapo ya kuchochea uchumi wa Viwanda.

Ad

Hayo yamesemwa leo Wilayani Lushoto, Mkoani Tangana Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu alipofanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai na kuzindua kituo cha Ubunifu cha kidijitali.

Dkt. Jingu amesema baada ya kutembelea miundombinu mbalimbali ya chuo na kuona hatua iliyofikiwa katika kuhakikisha Chuo hicho kinajikita katika kutoa wabunifu watakasaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu (mwenye Miwani) akipata maelezo kwa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Mabughai kuhusu mafunzo kwa vitendo katika fani ya umeme yanayotolewa na Chuo hicho kilichopo Wilayani Lushoto, Mkoani Tanga.

Amesema kuwa wataalamu wa ndani wanaweza kufanya mambo makubwa na kuondokana na utegemezi uvumbuzi kutoka nje ya nje na kutumia rasilimali zilizopo na kuoata teknolpjia itakayoendana na mazingira tuliyonayo.

Aidha, Dkt. Jingu amesema kiwa kituo cha Ubunifu cha kiditali Chuoni hapo kitumike kuchambua na kuendeleza mawazo ya kibunifu kwa kutumia sayansi na teknolojia ili kuweza kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Katika hatua nyingine, Dkt. Jingu amewataka wakazi wa Lushoto kutumia kauli ya Rais kuwa nchi yetu ya kwamba Nchi yetu ni Tajiri na haikubaliki Wananchi kuishi kwenye umasikini kwa kufanga kazi na kutumia rasilimali zilizopo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu (mwenye Miwani) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kituo cha ubunifu cha Kidigitali katika Chuo cha Maendeleo na Ufundi Mabughai, Lushoto Mkoani Tanga.

“Mbuni na kuwaza mambo ambayo yanaweza kuleta majawabu na kuleta unafuu wa maisha. Kituo hiki sio kwa ajili ya Wanafunzi pekee bali wananchi wanaozunguka chuo hiki” alisema

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO, Mhandisi Grace Daniel amewakata wananfunzi chuoni hapo kutumia kituo hicho kama fursa ya kuchakata mawazo waliyonayo kubuni mambo ambayo yanaweza kuwasaidia wanajamii kujikwamua kiuchumi.

“Hakika Kituo hiki kinaweza kuwa chachu ya kufikia malengo ya wabunifu na kutatua changamoto zinazotukabili katika jamii zetu” alisema

Mhandisi Grace amewataka wabunifu kuitumia SIDO kutatua changamoto zinazowakabili ili mawazo waliyonayo yanapelekwa mbele zaidi kwa maslahi ya Taifa.

Mwakilishi wa Wananchi wa Mabughai Malik Kupaza ameahukuru kwa jitihada za Serikali kuwezesha Tanzania kufikia uchumi wa Kati na kuwaomba wazazi na walezi kuwaleta watoto wao katika Chuo hicho kujifunza utaalam mbalimbali utakaowasaidia kujikwamua kiuchumi.

“Nakuomba Katibu Mkuu ufikishe salamu zetu kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli kwamba tunampongeza na tunamshukuru kwa kuletea kituo hiki”. Alisema.

Ameongeza kuwa wanatamani kuona mambo yanaingizwa katika matendo ili kuwezesha wanafunzi na wakazi wa maeneo jirani kuendeleza ubunifu.

Mpango wa maboresho ya miundombinu na teknolojia ya Chuo hicho utashirikisha Shirika la Viwanda Vidogo nchini, SIDO chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Chuo cha Mabhughai kilichoko chini ya Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *