Serikali ya Jimbo la Hunan nchini China imenzisha Mtaa Maalum wa kuuza kahawa kutoka Barani Afrika katika soko Kuu la Gaoquiao jijini Changsha. Hafla ya uzinduzi wa mtaa huo imefanyika na kuhudhuriwa na wawakilishi wa mataifa mawili yanayozalisha kahawa Tanzania na Ethiopia
Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mtaa wa Kahawa Mabalozi walipata fursa ya kutembelea migahawa inayouza kahawa kutoka Nchi za Tanzania, Ethiopia; Kenya na Rwanda, ambapo Mabalozi hao walipata fursa ya kukutana na Makampuni yanayonunua kahawa (whole sale buyers)
Hunan Galquiao Grand Market ni soko la (3) kwa ukubwa nchini China linalouza bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya China. Uzinduzi wa Mtaa wa Kuuza Kahawa kutoka Afrika ni sehemu ya hatua za Jimbo la Hunan kufungua soko lake kwa bidhaa kutoka barani Afrika.
Hafla ya ufunguzi wa Mtaa wa Kahawa ilifuatiwa na Mkutano wa biashara uliohudhuriwa na washiriki 360 (onsite) na 2000 (online) ambapo nchi za Tanzania, Ghana na Ethiopia zilipata fursa ya kuwasilisha mada juu ya fursa za biashara ya mazao ya kilimo na uwekezaji katika viwanda