KITUO KIKUU KIPYA CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI NA NCHI JIRANI CHA MBEZI LUIS JIJINI DAR ES SALAAM KIMEFANYIWA MAJARIBIO

Baadhi ya mabasi ya abiria yakiwa yamepaki katika kituo kipya cha mabasi cha Mbezi Luis jijini Dar Es Salaam ambapo kituo hicho kimefanyiwa majaribio
Baadhi ya mabasi ya abiria yakiwa yamepaki katika kituo kipya cha mabasi cha Mbezi Luis jijini Dar Es Salaam ambapo kituo hicho kimefanyiwa majaribio
Baadhi ya mabasi ya abiria yakiwa yamepaki katika kituo kipya cha mabasi cha Mbezi Luis jijini Dar Es Salaam ambapo kituo hicho kimefanyiwa majaribio

Kituo kipya Cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi Cha Mbezi Luis kimeanza rasmi majaribio leo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema kwa Sasa kituo hicho kinaweza kuanza kutumika Kutokana na miundombinu muhimu ya kituo kuwa Katika Hali mzuri.

Akizungumza wakati wa zoezi la majaribio lililowahusisha Askari wa usalama barabarani na Wadau wa vyombo vya usafiri, RC Kunenge ameshuhudia Mabasi yakiingia na kutoka pasipo usumbufu wowote.

Ad

Aidha RC Kunenge amesema kwa Sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya umaliziaji wa jengo na miundombinu mingine ambapo Hadi Sasa Ujenzi umefikia zaidi ya 90%.

Muonekano wa nje wa kituo kikuu kipya cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis jijini Dar es Salaam ambacho kimefanyiwa majaribio Novemba 25, 2020 na ujenzi wake ukiwa bado unaendelea.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo nao unaendelea vizuri chini ya Wakala wa TANROAD ambapo amewahimiza kuongeza kasi ili wakamilishe mradi mapema.

Hata hivyo RC Kunenge ameongeza kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha maagizo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka Ujenzi ukamilike mwishoni mwa mwezi huu yanatimia.

Kituo hicho kitakapokamilika kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba mabasi 1,000 na teksi 280 kwa siku, Pia kutakuwa na maeneo ya bodaboda na bajaji na eneo la mamalishe na babalishe, ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Novemba 30, 2020

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *