MAKATIBU WAKUU SADC -TROIKA WAJADILI HALI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA

Na Mwandishi wetu, Gaborone

Makatibu Wakuu wa SADC -TROIKA wamekutana na kujadiliana Mambo mbalimbali yakiwemo masala ya hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani ya SADC mjini Gaborone, Botswana.

Ad

Awali, Mkutano wa Makatibu Wakuu ulifunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Bw. Gaeimelwe Goitsemang ambae pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.

Ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC) kukutana ana kwa ana tangu ulipotokea ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (Covid-19).

Kwa upande wa Makatibu wakuu waliohudhuria katika Mkutano huo kutoka Tanzania ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.

Mkutano wa Makatibu Wakuu utafuatiwa na Mkutano wa Dharua wa Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama baadae leo mchana mjini Gaborone.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga zaidi ya shilingi bilioni 250 katika mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya msingi katika Halmashauri zote 184 nchini

Taarifa hii imetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *