WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU TOZO YA UNYAUFU, AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI MKURURGENZI MKUU BODI YA MAGHALA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Waendesha Maghala kuacha kukata tozo ya unyaufu kwenye zao la korosho kwa wakulima na wanunuzi kwa kuwa tozo hiyo imeshaondolewa na suala la unyaufu halijthibitishwa kitaalamu.


Ametoa agizo hilo Jumamosi (Novemba 18,2020) wakati wa kikao kati yake na Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi , Mtwara na Ruvuma, Makatibu Wakuu wa Wizara za  TAMISEMI, Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja Mrajisi wa Ushirika, Mtendaji Mkuu wa  Bodi ya Korosho, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya  Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maghala na Waendesha Maghala wote wa Mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi na Ruvuma, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Mkuu katika hatua nyingine amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maghala Bw. Odilo Majengo kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya Serikali kuhusu kusitisha tozo ya unyaufu katika zao la korosho.

Waziri Mkuu pia ametoa siku tano kwa waendesha maghala kuandaa taarifa kuhusu ni kiasi gani cha korosho ambazo wamechukua kutoka kwa wanunuzi wa Korosho kama tozo ya unyafu na atatuma timu maalum kwa ajili ya kazi hiyo.

Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *