BALOZI IBUGE ATAMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ETHIOPIA

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisaini kitabu cha wageni katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Ubalozi pamoja na kukagua mali za Serikali nchini humo.

Balozi Ibuge kabla ya kuanza kukagua mali za Serikali, alikutana na watumishi katika mkutano ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na uaminifu kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisisitiza jambo kwa watumishi (hawapo pichani) wakati wa mkutano

“Nawasihi sana kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake tufanye kazi kwa bidii na kuwa wabunifu wa kuitangaza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” Amesema Balozi Ibuge

Pamoja na Mambo mengine, Balozi Ibuge amewasihi Ubalozi huo kuhakikisha kuwa wanatekeleza vyema vipaombele vya Serikali ya awamu ya tano kama ilivyoelekezwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (2020 – 2025) katika Sura ya Saba, ambapo sura hiyo imeelekezwa kuwa Balozi zote kutekeleza Diplomasia ya Uchumi pamoja na Diplomasia ya Siasa.

Balozi Ibuge akipatiwa maelekezo kutoka kwa Afisa wa Ubalozi wakati wa ukaguzi wa mali zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania nchini Ethiopia

Pia Balozi Ibuge amekagua mali mbalimbali zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania nchini Ethiopia kwa lengo la kuijionea na kujiridhisha juu ya uwepo wa mali hizo.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Bibi Elizabeth Rwitunga amemhakikishia Balozi Ibuge kuwa watafanya kazi kwa umoja, bidii, weledi na ubunifu kwa maslahi ya Taifa.

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Bibi Elizabeth Rwitunga (mwenye gauni la rangi ya bluu) akimpatia maelezo Balozi Ibuge wakati alipokuwa akikagua mali zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania nchini Ethiopia

Na Mwandishi wetu, Addis Ababa

Bibi. Rwitunga ameongeza kuwa mashirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia ni mazuri na yanaendelea kuimarika ikiwemo ushirikiano katika masuala ya usafiri wa anga ambapo Shirika la Ndege la Ethiopia linashirikiana na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika masuala mbalimbali ikiwemo mafunzo na matengenezo ya ndege ambapo tayari watanzania watatu (3) wameshapatiwa mafunzo ya ndege.

Kuhusu Sera ya Diplomasia, Kaimu Balozi, Bibi. Rwitunga ameahidi kusimamia sera ya Diplomasia ya uchumi pamoja na Diplomasia ya siasa kwa kuhakikisha kuwa ubalozi utaendelea kuwasiliana na wawekezaji mbalimbali wa kuwekeza nchini Tanzania katika sekta za Nishati, Usafirishaji, Utalii pamoja na Biashara.

Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia unaiwakilisha Tanzania pia katika nchi za Djibouti, Yemen pamoja na Umoja wa Afrika na kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayosimamia masuala ya Uchumi Barani Afrika (UNECA).

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.