Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China hapa Nchini Mhe Wang Ke. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam.

CHINA NA TANZANIA KUSHIRIKIANA KIMKAKATI

China imesema itafanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2020 ili kuiwezesha Tanzania kupiga kwa haraka hatua za kimaendeleo kwa faida ya pande zote mbili.

Hayo yamo katika barua ya pongezi iliyotumwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yikwenda kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi iliyowasilishwa kwake na Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Wang Ke.

Ad

Akizungumza mara baada ya kukabidhi barua hiyo ya pongezi Balozi wa China hapa Nchini Wang Ke amesema China ina imani na Serikali ya Tanzania hususani mara baada ya uchaguzi mkuu uliomalizika mwezi octoba kwa utulivu na amani na kwamba imejipanga kuimarisha mahusiano ya kimkakati ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi kwa upande wake amesema anazipokea kwa unyenyekevu salamu hizo za pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yina kuongeza kuwa katika mazungumzo yake na Balozi Wang Ke wameangazia zaidi masuala mbalimbali nay a kimkakati ya kutekeleza hususani yale yanayolenga katika hotba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akilifungua bunge la 12 mjini Dodoma.

Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe Anders Sjoberg na baadae kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland hapa Nchini Mhe Riitta Swan na kuzungumzia namna ya Nchi hizo zitakavyoendelea kushirikiana katika nyanja za kiuchumi na kijamii ili kudumisha urafiki lakini pia kupiga hatua za kimaendeleo na kukuza uchumi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *