SERIKALI YA ZANZIBAR IMELENGA KUENDESHA NA KUKUZA UCHUMI WA BULUU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi ameuhakikishia uongozi wa Taasisi ya Aga Khan kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane inaweka taratibu na sheria nzuri za kuwavutia wawekezaji.

Rais Dk Hussein Mwinyi ameyasema hayo leo Ikuku Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Ujumbe wa Taasisi ya Aga Khan nchini Tanzania.

Rais Dk. Hussein alisema kuwa Serikali anayoiongoza itahakikisha inawawekeza mazingira mazuri wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambao wanalengo ya kuekeza Zanzibar katika sekta mbali mbali ikiwemo utalii, viwanda na nyenginezo.

Ad

Alisisitiza kuwa kipaumbe cha Serikali ya Zanzibar Awamu ya nane hivi sasa imelenga kuendesha na kukuza uchumi wa buluu kwa kuzitumia kikamilifu rasimali zinazohusiana na bahari, ikiwemo shughuli zinazohusu sekta ya utalii, utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi na bahari kuu, ufugaji na usindikaji wa samaki, ukulima wa mwani na nyenginezo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *