SHIDA YA MAJI KIBINDU KUWA HISTORIA – MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE

Mbunge wa Chalinze Ndg. Ridhiwani Kikwete amewahakikishia wananchi wa Kata ya Kibindu kuwa shida ya maji itabaki kuwa historia, akiongea mbele ya wananchi wa Kijiji cha Kwamduma, kata ya Kibindu Mh.Mbunge alimshukuru Mheshimiwa Rais na Serikali kwa hatua zinazochukuliwa kupata ufumbuzi wa shida ya maji katika kata hiyo.

Maneno hayo aliyatoa katika Mkutano huo wa wananchi uliohudhuriwa pia na wataalamu mbalimbali toka taasisi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Kawawa.

Ad

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya , Mh. Mbunge amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Mh. Raisi kwa hatua zilizokwisha fikiwa, Vilevile Mh. Mbunge alieleza kuridhishwa kwake na hatua mbalimbali zilizochukuliwa.

Kwa upande wake alieleza kuwa yeye kama Mbunge amefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuchimbwa kwa visima zaidi ya vinne katika vijiji mbalimbali vya kata hiyo ikiwemo Kwamduma visima viwili, kibindu viwili, na Kwamsanja kimoja ambavyo vimesaidia kidogo japo shida bado haijaisha.

“Uchimbaji wa mabwawa haya makubwa na usambazaji kwenda kwa wananchi unakuja wakati muafaka, hivyo matarajio ni kwenda kutatua shida ya Maji kwa ukubwa huo uliokusudiwa kwa hakika tuna kiongozi ambaye sio anasema mdomoni kuwajali wananchi wanyonge isipokuwa anatenda kwa vitendo pia” Amesema Kikwete

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Kawawa alieleza kuwa Serikali imejidhatiti kuhakikisha maji yanawafikia wananchi wa Kibindu hivyo alimuhakikishia Mbunge na wananchi kuwa mradi utakamilika mapema ili wananchi wapate maji safi na salama.

Akieleza juu ya Utekelezwaji wa miradi hiyo Mkuu wa Wilaya alieleza kuwa, tayari Serikali imetoa Bilioni 1.6 kwa ajili ya miradi yote ikiwemo Milioni 700 kwa ajili ya Kwamsanja na Milioni 900 kwa ajili ya Mjembe, Kwamsanja ambayo inatarajiwa kwa pamoja kutoa lita zisizo pungua Milioni Tatu na Nusu. Wingi ambao unakwenda kutatua kero ya Maji katika kata ya Kibindu.

Miradi hiyo itakapokamilika inataraji kuhudumia watu wanaoishi katika eneo la Kibindu na vitongoji vya kata za jirani.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *