MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA WAKANDARASI WANAWAKE NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekipongeza Chama cha Wakandarasi Wanawake Tanzania kwa kuweza kuunda umoja huo kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wadogo wadogo wanaomalizi vyuo hivi sasa.

 Amesema ni vyema kuwa na mkakati wa kuweza kuendesha Jumuiya hiyo vizuri ili wengi waweze kujiunga na Jumuiya hiyo na hasa kwa kuona mambo yote waliyoyapanga yanaweza kufanikiwa kwa vitendo.

Ad

Aidha Makamu wa Rais amewataka Wakandarasi hao Wanawake kujitahidi kuiweka na kuitunza vizuri Jumuuiya hiyo kwa vile Wanawake wengine walioko vyuoni wanawatizama wao kwa ajili ya kuweza kujiunga na Jumuiya hiyo.

Nae Rais wa Chama cha Wakandarasi Wanawake Tanzania Bibi Judith Udunga amesema lengo la kuonana na Makamu wa Rais ni kuiomba Serikali kuweza kuikopesha Mitambo Jumuiya hiyo ili iweze kupewa Miradi mikubwa pamoja na kuiomba Serikali iwasaidie Wakandarasi Wanawake kupitia Tanrod na Tarura.  

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *