MHANDISI NYAMHANGA ATOA SIKU 14 KUANZA KUTUMIKA KWA KITUO CHA MABASI MBEZI LUIS

Na. Angela Msimbira

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga ametoa siku kumi na nne kwa viongozi wa Mkoa wa Dar-es-salaam kuhakikisha kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha mbezi Luis kinaanza kutumika ifikapo Disema 20,2020

Akizungumza wakati wa zoezi la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo Mhandisi Nyamhanga amewataka kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maeneo yaliyobaki ili kuanza kutoa huduma za usafiri kwa jamii

Amefafanua kuwa kwa sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya umaliziaji wa majengo na miundombinu ya barabara ya kuingilia kwenye stendi hiyo, hivyo ni vyema wakaongeza kasi ya umaliziaji ili kituo hicho kianze kutumika kwa wakati.

Amesema kuwa kazi ya ujenzi wa Kituo hicho umekamilika kama ilivyoelekezwa na tarehe 1 desemba, 2020 msimamizi wa ujenzi ambaye ni kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi Dar-es-salaam kilitoa hati ya awali ya kukamilika kwa ujenzi kwa mkandarasi ambapo sehemu kubwa imekamilika , hivyo kituo hicho kipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma ya usafirishaji kwa jamii

Ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam kwa kuhakikisha wanasimamia ujenzi huo kwa weledi na kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati uliopangwa usimamizi na kuhakikisha kuwa kituo hicho kinakamilika kwa wakati

Mhandisi Nyamhanga ametoa maelekezo kwa uongozi huo kuhakikisha maandalizi muhimu yanafanyika kwa ajili ya kuanza kutoa huduma katika stendi hiyo ili huduma zinapoanza kutolewa kusiwepo na changamoto ambazo zinaweza kujitokeza

Aidha, amewaagiza Wakala wa Barabara TANROD kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo ili kuweza kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa jamii.

Vilevile, Mhandisi Nyamhanga ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuhakikisha wanaandaa mpango kabambe wa eneo lililopo karibu na stendi ili kutoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza kwenye ujenzi wa mahoteli na nyumba za kulala wageni ili kuwarahisishia wasafiri maeneo ya kufikia wanapokuwa safarini..

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *