PROF. SHEMDOE AILEKEZA TANTRADE KUANDAA MAONESHO YA BIDHAA ZA VIWANDA KILA ROBO YA MWAKA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelezo ya ufafanuzi muda mchache baada ya ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini,  05 Desemba 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere – Dar es Salaam.

Kongamano hilo lililenga kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki wa viwanda katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa nchini amabayo ni moja kati shughuli zilizopangwa kufanyika katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020

Ad

Prof. Shemdoe ametolea ufafanuzi wa utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa wakati akifungua Maonesho hayo ya kutumia maeneo ya uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere mara kwa mara si tu kwa maonesho ya sabasaba ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.Aidha, Prof. Shemdoe ameielekeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuweka maandalizi ya kuandaa maonyesho angalau kila roro mwaka ili watu wapate fursa za kuonesha, kutangaza na kuuza bidhaa zao ambazo zinazalishwa hapa nchini.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *