RAIS MAGUFULI AKAGUA MAENDELEO UJENZI WA OFISI ZA IKULU NA ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU JAJI MSTAAFU NSEKELA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo tarehe 08 Desemba, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Ikulu Mkoani Dodoma na kuelezea kuridhishwa na kiwango na kasi ya ujenzi wa majengo ya ofisi hizo unaofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mama Subilaga Nsekela, mjane wa aliyekuwa Kamishna wa Maadili Marehemu Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati wa kuaga mwili katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo Desemba 8, 2020

Ujenzi wa Ofisi hizo ulioanza tarehe 17 Februari, 2020 unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 3 ijayo na unafanywa kwa usanifu na muonekano sawa na Ofisi za Ikulu zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Ad
Rais Magufuli amewaongoza wananchi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Harold Nsekela aliyekuwa Kamishna wa Maadili, ambaye amefariki dunia tarehe 06 Desemba, 2020 Jijini Dodoma.

Msimamizi wa ujenzi wa ofisi hizo, Luteni Kanali George William Nyisa amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati uliopangwa.

Akikagua majengo yanayojengwa, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na uimara wa nguzo na kuta zinazojengwa na amesema ni fahari kubwa kwa Taifa kujenga ofisi yake ya Ikulu kwa kutumia Jeshi badala ya kutumia wakandarasi kutoka nje ya nchi.

Mhe. Rais Magufuli pia amezungumza na Vijana wa JKT wanaoshiriki ujenzi huo ambapo amekumbusha ahadi yake kuwa vijana hao 2,424 wataandikishwa katika JWTZ mara watakapomaliza jukumu la ujenzi wa Ofisi za Ikulu.

Rais Magufuli amewaongoza wananchi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Harold Nsekela aliyekuwa Kamishna wa Maadili, ambaye amefariki dunia tarehe 06 Desemba, 2020 Jijini Dodoma.

Pamoja na kuwapongeza vijana hao, Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza vijana wa kiraia wanaoshiriki katika ujenzi huo ambao ni mafundi, na amewaahidi kuwa atawaangalia mara baada ya kumaliza kazi hiyo.

Mapema leo asubuhi, Mhe. Rais Magufuli amewaongoza wananchi wa Dodoma kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Harold Nsekela aliyekuwa Kamishna wa Maadili, ambaye amefariki dunia tarehe 06 Desemba, 2020 Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Bw. Andendekisye Nsekela, mtoto mkubwa wa aliyekuwa Kamishna wa Maadili Marehemu Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati wa kuaga mwili katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo Desemba 8, 2020

Viongozi wengine waliotoa heshima za mwisho ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *