WAZIRI UMMY MWALIMU KUSIMAMIA MASUALA YA MUUNGANO NA MAZINGIRA YANAYOGUSA MAISHA YA WANANCHI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi yake (hawapo pichani) mara baada kupokelewa rasmi katika Ofisi za Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 9, 2020 katika Ikulu ya Chamwino.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu wake, Mhe. Mwita Waitara wakipokelewa rasmi katika katika Ofisi za Makamu zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 9, 2020 katika Ikulu ya Chamwino.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi yake mara baada kupokelewa rasmi katika Ofisi za Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 9, 2020 katika Ikulu ya Chamwino.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akisaini kitabu mara baada ya kuwasili Ofisini kwake katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 9, 2020 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo mara baada kupokelewa rasmi katika Ofisi za Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 9, 2020 katika Ikulu ya Chamwino.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu amesema atahakikisha utekelezaji wa majukumu ya kusimamia masuala ya Muungano na Mazingira yanagusa Maisha ya wananchi moja kwa moja kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.

Akizungumza na Menejimenti ya Ofisi yake mara baada kupokelewa rasmi katika Ofisi za Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma hii leo, Waziri Mwalimu amewataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo chanya kwa taifa.

Ad
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) na Naibu wake, Mhe. Mwita Waitara wakiwa katika mazungumzo na viongozi wa Ofisi hiyo mara baada kupokelewa rasmi baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 9, 2020 katika Ikulu ya Chamwino

“Tuna jukumu kubwa la kulinda na kuhifadhi mazingira pamoja na kudumisha muungano wetu ambao ni tunu ya Taifa letu” Alisisitiza Waziri Ummy Mwalimu.

Amesema ni muhimu kuendelea kuelimisha umma juu ya umuhimu wa Muungano kwa kushirikisha vijana ambao ni taifa na leo, hususan waliozaliwa baada ya muungano kwakuwa kuna mengi ya kujifunza.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mwita Waitara amesema kuwa atahakikisha kuna kuwa na ushirikiano baina ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika kusimamia kwa pamoja masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira nchini.

Waziri Ummy Mwalimu na Naibu wake Mwita Waitara hii leo wameapishwa rasmi kushika nyadhifa zao mara baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli 5 Desemba 2020.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *