HUNGARY NA TANZANIA ZATILIANA SAHIHI UFADHILI WA WANAFUNZI WA KITANZANIA

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Abdallah Possi akisaini makubaliano ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 wa Kitanzania Nchini Hungary.

Tanzania na Hungary zimetiliana saini makubaliano ya ufadhili kwa Wanafunzi zaidi ya 30 wa Kitanzania kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya Nchini Hungary katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2021 hadi 2023.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Ujerumani anayeiwakilisha pia Hungury Dkt. Abdalla Possi amesema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa Wanafunzi wa Tanzania kupata elimu katika Vyuo vya Hungary kwa masomo ya shahada ya kwanza,shahada ya Uzamili na shahada ya uzamivu katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma.

Ad
Balozi wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na maafisa wa Jamhuri ya Czech mara baada ya kusaini makubaliano ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 wa kitanzania nchini Czech.

Ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hungury na kwamba nafasi hizo zitaendelea kuongezeka kutokana na Serikali ya Hungary kufurahishwa na muitikio wa Watanzania wanaoomba nafasi hizo za masomo.

Katika tukio jingine Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani umefungua rasmi ofisi ya muwakilishi wa heshima wa Tanzania iliyoko katika mji wa Bruno katika nchi ya Jamhuri ya Czech.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemuidhnisha Bw. Roman Grolig kuwa mwakilishi wa heshima wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech ambapo mji wa Bruno ni mji wa kimkakati ambapo kila mwaka mamlaka za mji huo huandaa miongoni mwa mambo mengine maonesho makubwa ya biashara na utaliibarani Ulaya.

Mji wa Bruno pia ni makao makuu ya Baraza la biashara la Czech – Tanzania.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *