SERIKALI KUENDELEA KUTATUA KERO ZA MIPAKA CHALINZE – KIKWETE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amewahakikishia wananchi wa Kata ya Pera na Chalinze kuwa Serikali itaendelea kutatua kero za migogoro ya Ardhi katika Halmashauri hiyo wakati wa ziara ya kukutana na kuwashukuru Wananchi wa jimbo hilo kufuatia ushindi mkubwa walioupata.

Akiongea na wananchi wa Kata ya Pera , Mbunge aliwahakikishia wananchi kuwa wamejipanga vizuri kumaliza kero za mipaka hasa ile isiyokwisha kati ya Kitongoji cha Pingo na Chamakweza ambao umedumu kwa takribani miongo miwili.

Ad
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi

Awali akiwa katika Kitongoji cha Pingo, Mbunge alifanya mkutano wa wazi na Wananchi ambapo pia aliongozana na watalaam mbalimbali wa Idara pamoja na viongozi wa ngazi ya Vitongoji, Kata na Wilaya wakiwemo Wanasiasa.

Mbunge amewaahidi Wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano huku akiwashukuru kwa kukichagua kura nyingi Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo kumpatia asilimia zaidi ya 94 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akimsikiliza mwananchi wa jimbo hilo

Katika mkutano huo ambao Mbunge alipokea pia kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi ikiwemo migogoro wa mipaka,
Mgorogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji, Fursa za TASAF, mikopo ya Jamii , Afya na mengineyo.

Hata hivyo Mbunge ametoa ufafanuzi baadhi ya kero za Wananchi ambazo zimeanza kufanyiwa kazi na kuwakumbusha kuwa serikali haikuwa imelala na kwamba inafanya kazi, huku zingine akiahidi kuzichukua kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *