WAZIRI BASHUNGWA: TUNATAKA MIPANGO NA MIKAKATI YA VYAMA VYA MICHEZO, KAZI IMEANZA

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, amemwaleza Waziri Mstaafu wa Wizara hiyo, Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa yeye na Naibu wake, Abdallah Ulega, wameanza kazi mara na moja ya mageuzi watakayoyaendeleza ni kutaka kuona michezo inakuwa na mchango zaidi.

Waziri Bashungwa ameyaeleza hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akikabidhiwa rasmi ofisi na Dkt. Mwakyembe. Amesisitiza msimamo wa Wizara hiyo wa tangu awali kuwa vyama na mashirikisho yote ya michezo nchini kuwasilisha mipango na mikakati yao kufikia Disemba 31 mwaka huu.

Ad
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hassan Abbas

Awali akitoa salaam kwa niaba ya wafanyakazi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, aliahidi kuwa Wizara hiyo ilifaidika mno na ujuzi wa Dkt. Mwakyembe na wataendeleza maono yake mazuri.

“Najua mengine huwezi kujisemea lakini unepush sana kuonekana kwa Wizara hii, umesaidiana nasi kutekeleza sheria za habari na pale TBC kuna kampuni ya ubia na Wachina uliniteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kutatua Changamoto na leo hii unaondoka pale kampuni ile iliyokuwa ikipata hasara kwa miaka kumi mwaka huu imetoa gawio na pesa nyingine kwa TBC zaidi ya Bilioni 3,” alisema Dkt. Abbasi.

Waziri Bashungwa na Naibu wake wamemwahidi Dkt. Mwakyembe kuwa wamekuta treni katika wizara hiyo likiwa limeshika kasi, wao wataongeza tu kasi zaidi.

“Mimi hapa nauona mwanga tangu nifike. hii ni wizara ambayo ni roho ya nchi. Mzee wetu Mwakyembe jua kwamba sisi tutaendeleza ulipoishia na hatutasita kukualika kutushauri jinsi ya kwenda zaidi,” alisema Waziri Bashungwa.

“Sisi tunakushukuru sana kwa kutuachia watendaji wenye uzoefu mkubwa na sekta hizi na kama ulivyosema walikusaidia sana, nasi tunaamini watatusaidia sana pia kufikia maono ya Ilani ya Uchaguzi lakini pia na maono ya Mhe. Rais,” aliongeza Naibu Waziri Ulega.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *