TANZANIA NA PAKISTAN ZASAINI MIKATABA YA MAKUBALIANO YA KIDIPLOMASIA

Tanzania na Pakistan zimetiliana saini mikataba miwili ya makubaliano ambayo ni mkataba wa mashaurino ya kidiplomasia pamoja na mkataba wa kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano wa kiuchumi.

Mikataba hiyo imesainiwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akiangalia baadhi ya nyaraka alizokabidhiwa na Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa makubaliano hayo yanatoa fursa nyingi zilizopo za kuongeza na kukuza biashara kati ya Tanzania na Pakistan hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite, pamoja na uwekezaji.

“Tanzania na Pakistan zina uhusiano wa muda mrefu na katika mazungumzo yetu ya leo, Balozi wa Pakistan ameeleza fursa zilizopo Pakistan ambapo fursa hizo zikitumiwa vizuri zitanufaisha mataifa yote mawili,” Amesema Prof. Kabudi 

Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi kabla ya kusainiwa kwa mikataba ya makubaliano Jijini Dar es Salaam
 

Prof. Kabudi ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Pakistan na kwamba fursa hizo zitaendelea kuongeze ushirikiano wa diplomasia ya uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.

Kwa Upande wake Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem amesema kuwa kusainiwa kwa mikataba hiyo muhimu itasaidia kukuza na kuendeleza diplomasia ya Uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem wakisaini mikataba ya makubaliano katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

“Ni imani yangu kuwa kusainiwa kwa mikataba hii miwili ya makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Pakistan kutasaidia kudumisha na kukuza uchumi kati ya mataifa yetu,” Amesema Balozi Saleem

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.