RAIS WA ZANZIBAR DKT. MWINYI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI ELIAS KUANDIKWA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias Kuandikwa kwa uteuzi alioupata na kuahidi kuendelea kushirikiana nae.

Rais Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias John Kuandikwa aliyefika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha na kumsalimia Rais ambapo pia, Waziri huyo alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Faraji Mnyepe.

Ad

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Hussein Mwinyi alieleza jinsi alivyofarajika na uteuzi wa Waziri huyo kutokana na uwezo wake mkubwa wa uongozi na kuahidi kumpa mashirikiano makubwa ili iwe ni chachu katika utekelezaji wa kazi zake ndani ya Wizara hiyo.

Rais Dk. Hussein alisema kuwa kwa vile Wizara hiyo ni ya Muungano ana matumaini makubwa kwamba ataendelea kuwa karibu na Waziri huyo katika kuhakikisha anatekeleza vyema majukumu yake sambamba na kuhakikisha Brigedi za Zanzibar zinaendelea kuimarika zaidi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *