Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Wizara ya Madini kilichofanyika katika Mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma tarehe 11 Disemba 2020.

WAZIRI BITEKO AFUTA LESENI SITA ZA WAFANYABIASHARA WA MADINI CHUNYA

Na, Tito Mselem, Chunya

Waziri wa Madini Doto Biteko, amefuta leseni Sita za wafanyabiashara wa madini ya dhahabu ambao wanatuhumiwa kujishughulisha na utorashaji wa madini wilayani Chunya.

Ad

Watuhumiwa hao, wametakiwa kutojishughulisha na shughuli yoyote ya Madini nchini.

Wakati huo huo, Waziri Biteko, ameagiza kuondolewa kwa Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Madini ya dhahabu anaye husika na usimamizi wa Soko la Madini la Chunya Gagala Poul.

Vile vile Waziri Biteko amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Ofisi ya Madini wa Mkoa wa kimadini wa Chunya baada ya kutuhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara kutorosha madini, ambao watumishi hao ni Gabliel Masai, Edward Gavana na George Wandiba.

Pia, Waziri Biteko, ameagiza kusajiliwa kwa Mialo yate inayo chenjua madini ya dhahabu wilayani Chunya ili kujua mwalo gani umezalisha kiasi gani cha dhahabu na dhahabu hiyo imepelekwa kuuzwa soko gani.

“ Bora tubaki na wanunuzi wawili wa madini ya dhahabu ambao ni waanifu kuliko kuwa na mlolongo wa wanunuzi ambao sio waaminifu na wasio fuata kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa,” amesema Waziri Biteko.

Waziri Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila kutoa zawadi wale wote watakao saidia kupatikana kwa watu wanao torosha madini.

“Niwaombe wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kukomesha tatizo la utoroshaji madini, tunataka nidhamu kwenye sekta ya madini ili tulete tija na maendeleo nchini,” amesema Waziri Biteko. 

Pia, Waziri Biteko, amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini nchini kuhakikisha wanapeleka madini yao sokoni na kuachana na ufanyaji biiashara ya madini nje ya masoko ya madini.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amempongoza Waziri wa Madini kwa kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bukombe na kuteuliwa tena kuwa Waziri wa Madini.

Pia, Chalamila amesema tayari Serikali imeanza kujenga gereza ili watu watakao kamatwa wakitorosha madini hawatapekwa mbeya mjini bali watafungwa katika gereza hilo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *