WAZIRI KABUDI AHIMIZA USHIRIKIANO MIONGONI MWA NCHI ZA OACPS

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi ambaye pia Rais wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pasific (OACPS) jana tarehe 14 Disemba, 2020 amefungua na kuongoza Mkutano wa Jumuiya hiyo ambao uanatarajiwa kufanyika kwa kipindi cha siku tatu.

Umoja huu wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific wenye nchi Wanachama 79 ulianzishwa pamoja na mambo mengine, kuweka misingi ya majadiliano na nchi za Ulaya katika maeneo mbalimbali yenye maslahi kwa nchi wanachama kama vile mikataba ya biashara, ulinzi na usalama wa watu na rasilimali. 

Ad

Akizungumza muda mfupi baada ya kufungua mkutano huo Pro. Kabudi alisema Nchi Wanachama wa OACPS kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea hivi sasa Duniani na hasa katika nchi za Ulaya ambayo yanazipunguzia nchi hizo nafasi ya kuendelea kusaidia nchi zingine, na kwakuzingatia kuwa Uchumi wa nchi wanachama wa OACPS katika kipindi cha miaka 45 ya Umoja umekuwa, ni wakatika muafaka kwa Jumuiya hiyo kuimarisha zaidi ushirikiano wake. Hatua hii itaifanya Jumuiya hiyo sio tu kufikiria namna ya kufanya biashara na nchi za Ulaya bali kufikiria zaidi namna ya kukuza biashara miongoni mwa nchi Wanachama wenyewe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa na ujumbe wa Tanzania alipokuwa akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS). Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Mhe. William Tate Ole Nasha, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe. Jestas Abouk Nyamanga, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwanaid Ali Hamis

Kwa upande mwingine Prof. Kabudi amezitaja baadhi ya agenda zitakazojadiliwa katika mkutano huu wa siku tatu kuwa ni pamoja na nchi za OACPS kujadali namna ya kukuza na kuboresha Ushirikiano, kuongeza Wadau wake kama vile nchi za BRICS na kufanya mapitio ya mkataba mpya wa ushirikiano kati ya Nchi za Africa, Caribbean, Pasific na Ulaya kwa kuwa Mkataba wa sasa (Cotonou Partnership Agreement) unafikia kikomo. “wakati umefika sasa kwa Jumuiya hii kuongeza wadau, kushikamana na kusimama pamoja katika masuala muhimu ya kidunia kwenye jukwaa la Umoja wa Kimataifa.” Prof. Kabudi. Aliongeza kuwa agenda nyingine itakayo jadiliwa nikuhusu muundo mpya wa Sekretarieti ya Jumuiya unalolenga kuongezea uafanisi zaidi na kupunguza gharama za uendeshaji. 

Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Makutano wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS).

Mkuatano huu vilevile unatarajiwaa kujadili masuala mbalimbali ya biashara baina Afrika, Caribbean, Pasific na nchi za Jumuiya ya Ulaya likiwemo suala viwango vipya vya ushuru wa mazao ya samaki ambayo nchi Wanachama wa OACPS zimekuwa zikiuza kwenye soko la Ulaya.

Sekretarieti ya OACPS wameipongeza Tanzania kwa uongozi mahiri na ushirikino waliouonyesha katika kipindi cha miezi sita (6) ambayo imekuwa Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo. Nafasi hii ya Urais inashikiliwa na Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi hadi tarehe 31 January 2021. 

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA SULUHU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA NCHI, WIZARA YA MAMBO YA NJE YA SHIRIKISHO LA JAMHURI YA UJERUMANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na kuagana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.