RC KUNENGE AWATAKA MANISPAA KINONDONI NA JKT KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA DALADALA MWENGE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameitaka Manispaa ya Kinondoni na mkandarasi kutoka JKT kuhakikisha Ujenzi wa kituo Cha daladala Mwenge na Maduka 126 vinakamilika kabla ya February 28 na kuanza kutumika Machi 01 ili kiweze kutoa huduma kwa wananchi Kama ilivyokusudiwa.

RC Kunenge ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kukagua miradi Wilaya ya Kinondoni ambapo amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anampatia mkandarasi fedha kwa wakati ili mkandarasi asipate kikwazo Cha kumfanya ashindwe kutekeleza agizo hilo.

Ad

Aidha RC Kunenge amewaelekeza Wakurugenzi wa Manispaa zote za jiji hilo kuhakikisha ifikapo February mosi masoko yote yaliyokamilika yanaanza kutoa huduma kwakuwa lengo la Ujenzi wa masoko ilikuwa ni kutumika na sio kubaki Kama magofu Jambo linalopelekea Serikali kukosa Mapato na wafanyabiashara kuendelea kubanana mitaani.

Akiawa kwenye Ujenzi wa Kiwanja Cha Mpira Cha KMC na Maduka 79 RC Kunenge amewaelekeza JKT kuongeza kasi ya Ujenzi wa Kiwanja hicho na kusema kuwa anachokitaka ni kuona ifikapo February mosi Maduka yote 79 yanakuwa tayari yamekamilika na yamepata wapangaji.

Hata hivyo RC Kunenge ametembelea Ujenzi wa Barabara za DMDP eneo la Bwawani na ujenzi wa Soko la Bwawani linalojengwa pia na DMDP na kuelekeza ifikapo Disemba 31 mwaka huu Soko liwe limekamilika na Mara baada ya kukamilika lianze kutumika ambapo amesesitiza Manispaa ya Kinondoni kuhakishisha wanaostahili kupata nafasi ya kufanya Biashara wanapatiea na Kodi ya pango iwe nafuu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA RAIS WA JAMHURI YA KENYA DKT. WILLIAM SAMOEI RUTO, NAIROBI NCHINI KENYA

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.