SIMAMIENI MIRADI YA MAENDELEO – NAIBU WAZIRI SILINDE

Na Angela Msimbira SUMBAWANGA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa David Silinde amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia kikamilifu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri zao ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati

Naibu Waziri Silinde ametoa agizo hilo, leo kwenye ziara yake ya Kikazi kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Akikagua miundombinu ya kituo cha afya cha Mazwi, Manispaa ya Sumbawanga Mhe. Silinde amepongeza usimamizi mzuri uliofanywa na Halmashauri hiyo kwa usimamizi wa ujenzi wa kituo hicho ambacho kwa sasa kimeanza kutoa huduma kwa jamii

“Nimeridhishwa na ujenzi wa Kituo cha afya cha Mazwi, kimejengwa vizuri na thamani ya fedha na majengo inaonekana, toenihuduma bora za afya kwa jamii ili waweze kuvutiwa na huduma zinaotolewa katika vituo vilivyokarabatiwa na kujengwa na Serikali” amesisitiza Mhe. Silinde

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha fedha zinazotolewa zinaenda sambamba na thamani ya miradi inayotekelezwa katika Halmashauri, hivyo ni vyema kuhakikisha zinasimamia kwa karibu ukamilishaji wa miradi yote ili ianze kutoa huduma kwa kwa wakati uliokusudiwa na Serikali.

“Utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri na ukamilishaji wake kwa wakati utasaidia kuleta maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla lengo likiwa ni kutoa huduma bora kwa wananchi” amesisitiza Mhe. Silinde

Wakati huohuo Mgannga Mkuu wa Manispaa ya Sumbawanga Dkt. Archie Hellar amesema Kituo cha Mazwi ni miongoni mwaa vituo 44 vilivyopata kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Hiller anaendelea kufafanua kuwa hadi sasa huduma zinazotolewa ni huduma ya wagonjwa wa nje, huduma za mama na mtoto, huduma za upasuaji, mionzi, maabara, kiliniki ya baba, mama na mtoto, huduma ya ushauri nasaha na uanzishwaji wa duka la dawa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *