WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI WAFANYA ZIARA KWENYE MRADI WA JULIUS NYERERE (JNHPP)

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato wamefanya ziara kwenye ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwa ajili ya kujionea utekelezaji wa mradi ambao utazalisha umeme wa megawati 2115.

Ziara hiyo iliyofanyika, tarehe 14 Desemba, 2020 iliwahusisha Naibu Katiku Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi leonard Masanja, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Edward Ishengoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco, Dkt. Alexander Kyaruzi, Mkurugenzi Mtendaji Tanesco, Dkt. Tito Mwinuka na wataalamu mbalimbali kutoka katika Wizara ya Nishati na Taasisi zake.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada kumaliza kukagua mradi huo, Waziri Kalemani amesema kuwa , Serikali imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi huo, ili kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi katika mradi huo.

“Tunataka mradi ukamilike kwa wakati na kwa kiwango cha juu, sio mradi unakamilika baada ya miezi miwili unanza kuhitaji tena ukarabati kwa gharama nyingine kwa hili hatutakubali kwa hiyo nitoe wito kwa mkandarasi kufanya kazi kwa weledi na kiwango cha juu” alisema Dkt. Kalemani

Ad

Dkt. Kalemani pia ametoa maagizo kwa mkandarasi pamoja na msimamizi wa mradi huo, kuwa amesitisha likizo za sikukuu za krimasi na mwaka mpya na watumie muda huu kufanya kazi kwa kasi ili mradi huo ukamilike kwa wakati.

Pia, amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha kuwa wataalamu wote ambao wanahitajika kwenye mradi huo wafike mara moja kwenye mradi huo ili kazi zifanyike kwa haraka.



Vilevile, amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anajiri waatalamu wote ambao wanahitajika katika ujenzi wa mradi huo na ifikapo mwisho wa mwezi huo wawe tayari wamefika nchini kwaajili ya ujenzi huo.

Dkt. Kalemani aliongeza kuwa, mradi wa Julius Nyerere utapeleka umeme kwenye gridi ya Taifa pamoja na kwenye miundombinu yenye uhitaji wa umeme kwa gharama nafuu.

Pia umeme huo utapelekwa kwenye vijiji 12,0268 Nchi nzima pamoja na kwenye Vitongoji vyake.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *