KATIBU MKUU MWAKALINGA AWATAKA NCC KUJITANGAZA

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi NCC, Dkt. Matiko Samson Mturi akizungumza kwenye Kikao cha Tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa NCC lilichofanyika jijini Dar.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NCC wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Arch. Elius Mwakalinga kwenye kikao hicho.
 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Arch. Elius Mwakalinga amewata Menejimenti na Watumishi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kutangaza kazi wanazozifanya ili zieleweke kwa jamii na kuongeza wigo mpana wa kuwahudumia wananchi.

Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa NCC jijini Dar, Arch. Mwakalinga amesema huu ni wakati wa Baraza hilo kushirikiana na taasisi nyingine katika sekta ya ujenzi ili kuboresha huduma za ujenzi na kufanya gharama za ujenzi nchini kuwa za bei nafuu.

Ad

“…Hakikisheni gharama za ujenzi nchini zinakuwa nafuu na zinazotekelezeka ili kuvutia watu kuwekeza katika ujenzi kwa kuwaelimisha fursa zilizopo na kutatua migogoro ya ujenzi kwa wakati,” amesema Arch. Mwakalinga.

Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NCC jijini Dar es Salaam
 

Aidha amemtaka Mtendaji Mkuu wa NCC, Dkt. Matiko Samson Mturi kuhakikisha watumishi waliopo katika baraza hilo wanakuwa na elimu, ujuzi na umahiri ili tafiti zinazofanywa ziweze kuwa na tija kwa taifa kwa muda mrefu.

“..Hakikisheni kuwa hamuwi wanyonge kwa kuwaendeleza kitaaluma watumishi wenu, kutangaza kazi kubwa mnazozifanya ili jamii izifahamu na kunufaika nazo na kufanya tafiti zinazoleta unafuu wa maisha kwa jamii ikiwemo kutayarisha wataalam wa ushuluhishi wa masuala ya ujenzi,” amesisitiza Katibu Mkuu, Arch. Mwakalinga.

Naye Mtendaji Mkuu wa NCC, Dkt. Matiko Mturi amesema kati ya mwaka 2018 hadi 2023 baraza limejipanga kuhakikisha migogoro mingi ya ujenzi inatatuliwa huku wadau wa ujenzi wakielimishwa ili kuepuka migogoro.

“…Tumejipanga kuhakikisha tunaboresha idara ya utafiti ili masuala mengi yanayoamuliwa na baraza hilo yawe ni matokeo ya tafiti za kina, ambayo yatakuwa hayajirudii mara kwa mara,” amesema Dkt. Mturi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Awakaribisha Wawekezaji Katika Nishati ya Jotoardhi Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewakaribisha wawekezaji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *