WATAALAM WA TIBA ASILI WATAKIWA KUFANYA UTAFITI WENYE USHAHIDI

Wataalam wa tiba asili na tiba mbadala nchi wametakiwa kufanya utafiti ambao utakuwa na ushahidi wa usalama wa dawa pamoja na ufanisi wa wa dawa hizo kwa watumiaji.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto-Idara kuu Afya Bw. Edward Mbanga wakati wa kikao cha pamoja cha wizara na wataalam hao kutoka taasisi za Serikali na Vyuo Vikuu mbalimbali nchini kilichofanyika kwenye ukumbi wa wizara jijini Dodoma.

Ad

Mbanga amesema kuwa ushahidi huonekana kwenye utafiti hivyo warudi nyuma na kujiuliza wamekosea wapi na nini kifanyike ili kuwa na uelewa wa pamoja kwani kizazi kijacho kinahitaji kuelezwa na kuelewa tiba asili.

Washiriki wa kikao kazi cha siku mbili cha kujadili muelekeo wa tiba asili nchini kinachofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za wizara zilizopo Area D jijini Dodoma

“Lazima tuulizane tunataka kufikia wapi na kuweka mikakati ya kuyafikia,nashauri tutambue nini kifanyike,tuna changamoto zipi na tunafikaje huko kwa kushirikiana kwa pamoja ili tutambue kwanini hatufiki hivyo lazima tujikite kwenye utafiti wenye ushahidi”.Alisisitiza.

Aliongeza kuwa katika kikao hicho wataalam hao wanatakiwa kutafuta majibu ambayo tiba asili itaendelea hata baada ya kipindi hiki,na wawe na matamanio kama nchi nyingine ili tiba asili itolewe kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Wataalam wa tiba asili/mbadala wakifuatilia hotuba ya ufunguzi toka kwa Kaimu Katibu Mkuu-Idara kuu Afya

“Tumekuwa tukifanya utafiti wa masuala ya tiba asili na tiba mbadala kuanzia miaka ya sitini, sasa tujiulize tangu tutafiti hadi sasa matokeo yanafanana?,bado kuna changamoto ya watu kushindwa kuthamini vya kwao hasa katika matumizi ya tiba asili kwa kuamini vinavyotoka nje ya nchi vina ubora zaidi kuliko vya kwao.

Hata hivyo Kaimu katibu mkuu huyo aliwataka katika kikao hicho watoke na mkakati wa kuanzisha vituo vya uendelezaji vya tiba asili kwenye halmashauri zote kwa kuwapatia ujuzi na motisha wataalam wa tiba asili pamoja na kufanyia tafiti dawa zao na mwisho wa utafiti kuwe na haki miliki.

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa kikao kazi cha kujadili muelekeo wa tiba asili na tiba mbadala nchini.

Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mguu wa Serikali Dkt. Eliud Eliakimu amesema kuwa kama nchi wameamua kuendeleza tiba asili kwa umoja ili kuwe na spidi ambayo italeta mafanikio yenye tija nchini.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Tiba kutoka Wizara ya afya Dkt. Grace Maghembe amesema tiba asili zipo na zinatumika kutibu magonjwa mbalimbali na malighafi ya kutengeneza dawa hizo zipo hapa nchini hivyo uwezo wa kutengeneza katika viwango kama nchini nyingine inawezekana endapo kutawekwa msukumo na hivyo kusaidia kuinua uchumi wa nchi na wa wakulima wa hapa nchini.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *