HOSPITALI YA SANITAS YAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WAKE

Hospitali ya Sanitas yapewa siku saba kukamilisha malimbikizo ya mishahara kwa watumishi wake agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana Patrobas Katambi mara baada ya kuzuru ofisini hapo kwa lengo la kujiridhisha na masuala ya kisera yanayohusiana na ajira, kazi na vijana.

Akiwa ofisini hapo, Naibu waziri amebaini watumishi wa Hospitali hiyo kutokupatiwa stahiki zao za kiutumishi ikiwemo mishahara yao kwa kipindi cha miezi 13 sasa kwa kigezo cha kuyumba Biashara kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Ad

Katambi amesema kulipa mishahara watumishi ni takwa la kikatiba na haliwezi kuvunjwa kwa kigezo chochote kile, hasa ikizingatiwa kaulimbiu ya wizara kwa awamu hii ni “mtumishi alipwe ujira wake kabla jasho halijakauka” lengo likiwa kuhakikisha kwamba mfanyakazi mtanzania anapata haki yake kwa wakati na kulinda ajira za wazawa.

“Watumishi Hawa wanamahitaji binafsi, wanafamilia zinawategemea na wanatakiwa kulipa Kodi za serikali kupitia mishahara yao, kitendo cha ninyi kutowapa mishahara yao kipindi chote hiki sio tuu kuwakoseshea mahitaji yao ya msingi bali mnakwamisha pia Kodi za serikali”
Ameongeza Naibu Waziri

Aidha Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi wa Sanitas kuwapa mikataba isio na ukomo watumishi wanaostahili mikataba hiyo, kuwe na vyama vya wafanyakazi, kuwasilisha nyaraka zinazohusu umiliki wa kampuni ili ziweze kupitiwa upya pia Uongozi uwe na sera mbalimbali hususan ya ajira na ukimwi Ili ziweze kufuatwa kikamilifu katika majukumu ya kiutawala.

Kwa upande wake kamishna wa Ajira Nchini Tanzania Brigedia Mbindi amesema ziara hii ni endelevu kwa nchi nzima lengo likiwa ni kuhakikisha sheria na miongozo mbalimbali ya kazi inafuatwa kikamilifu na wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira bora.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo amesema Kinondoni inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili waajiriwa wa sekta binafsi hivyo kwa ziara hii kutapunguza changamoto kwa waajiriwa na kuwapa mazingira mazuri wawekezaji katika kutimiza majukumu yao.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri amepongeza uongozi wa kiwanda cha coca-cola kwanza kwa kufuata kikamilifu sheria za kazi hususan Katika kuwapa kipaumbele wafanyakazi wazawa na kuwapatia mafunzo wazawa Katika yale maeneo ya utaalamu.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri ametembelea Hospitali ya Sanitas iliyopo Mikocheni na Kiwanda cha coca-cola kwanza.

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *