DAWASA WATEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT. MAGUFULI LA KUFIKISHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA, KIFURU NA SEGEREA

Kufuatia agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kufikisha huduma ya Maji safi kwa wakazi wa Jimbo la Ukonga na Segerea kabla ya Disemba 25 Mwaka huu, hatimae DAWASA wametekeleza agizo hilo.

Mapema leo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amejionea ukamilishaji wa Mradi wa Ujenzi wa Tank kubwa la Maji linalopokea maji kutoka Kisarawe kwenda Pugu lenye uwezo wa kupokea na kusambaza Lita milioni 2.8 kwa siku Wenye thamani ya shilingi bilioni 6.9 ambapo tank hilo leo limeanza kupokea maji na kuyasambaza kwa wananchi.

Ad

Mradi huo utahudumia wakazi wa Jimboa Ukonga ikiwemo Pugu, Majohe, Gongolamboto, Bangulo, Airwing, Kigogo, Chanika, Kinyamwezi, Banana, Segerea na Kifuru.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa wito kwa wananchi kulipa bili za Maji ili kuiwezesha DAWASA kuendelea kupanua huduma.

Aidha RC Kunenge amesema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wezi wa maji na wanaoharibu miundombinu ya Maji huku akiwaelekeza DAWASA kudhibiti tatizo la upotevu wa Maji.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji
Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *