TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KIDUNIA NA YA KWANZA AFRIKA MASHINDANO YA TEHAMA

Waziri wa Mawasiliano na Teknollojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya TEHAMA ambapo Tanzania imeshika nafasi ya pili kidunia na ya kwanza Afrika. Tuzo hizo zimetolewa Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa mgeni rasmi

Tanzania imeshika nafasi ya pili kidunia na ya kwanza katika bara la Afrika katika mashindano ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa mwaka 2020 yanayoratibiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania katika vituo 14 vilivyopo kwenye vyuo vikuu nchini Tanzania

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizungumza kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kutoa tuzo kwa washindi wa mashindano ya TEHAMA ambapo Tanzania imeshika nafasi ya pili kidunia na ya kwanza katika bara la Afrika

Ad
Waziri wa Mawasiliano na Teknollojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, mgeni rasmi kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa mashindano ya TEHAMA ambapo Tanzania imeshika nafasi ya pili kidunia na ya kwanza Afrika. Tuzo hizo zimetolewa Dar es Salaam

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ushindi huu unaakisi ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kutambua mchango wa TEHAMA katika kuendesha Serikali na kuhudumia wananchi wake; kukuza uchumi; na kuchangia pato la taifa katika kipindi hiki cha Mapinduzi ya Nne ya Viwanda na uchumi wa kidijitali

Ameongeza kuwa uundaji wa Wizara hii mpya utawezesha kuratibu na kusimamia masuala ya TEHAMA nchini ili kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na kutumia vema TEHAMA kwa kuwa ukiwekeza kwa asilimia 10 kwenye TEHAMA unaongeza pato la taifa kwa asilimia 1.5

Waziri wa Mawasiliano na Teknollojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (aliyeketi katikati), mgeni rasmi baada ya hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa mashindano ya TEHAMA (waliosimama nyuma) ambapo Tanzania imeshika nafasi ya pili kidunia na ya kwanza Afrika. Tuzo hizo zimetolewa Dar es Salaam

Akihutubia washindi hao na wadau wengine, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imedhamiria kufikisha miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye maeneo mengi zaidi nchini kwa lengo la kuongeza matumizi ya mawasiliano ya kasi ya brodibandi kutoka asilimia 45 ya sasa hadi kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2025

Amefafanua kuwa ili kufikia malengo hayo, Serikali itatoa kipaumbele kwenye masuala ya utafiti na ubunifu sanjari na kuwatambua na kuwasajili wataalamu wa TEHAMA nchini ili kuwa na wataalamu wa kutosha kwenda sambamba na ukuaji na mabadiliko ya teknolojia duniani

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa mashindano ya TEHAMA ambapo Tanzania imeshika nafasi ya pili kidunia na ya kwanza Afrika.

Na Prisca Ulomi, WMTH

Pia, amezitaka kampuni za ndani zinazojishughulisha na masuala ya TEHAMA ziige mfano wa kampuni ya HUAWEI kwa kuwekeza zaidi kwa kundi la vijana kwa nia ya kuibua na kuendeleza vipaji. Pia, ametoa wito kwa wananchi kutumia vizuri TEHAMA katika shughuli za uzalishaji mali na na utoaji huduma katika sekta mbali mbali ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo HUAWEI kuhakikisha kuwa inaendelea kuanzisha vituo vya umahiri vya sayansi na teknolojia kwenye taasisi za elimu ya juu nchini kwa kuzingatia maeneo ya kimkakati katika kujenga uchumi imara

Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA DAR ES SALAAM INAPANUKA NA KUIMARIKA: HATUA MUHIMU KWA UCHUMI WA TANZANIA

Bandari ya Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha biashara na uchumi wa Tanzania, na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *