GEKUL AWATAKA WAFUGAJI KUWA WAZALENDO

Mkurugenzi wa kiwanda hicho Shabbir Virjee akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Mifugo Pauline Gekul katika Ziara maalum kiwandani hapo ili kujionea uendeshaji wa kiwanda hicho.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Pauline Gekul amewataka wafugaji haswa wa Kanda ya Kaskazini, kuhakikisha kuwa wanauza Mifugo yao katika kiwanda Cha Eliya food Overseas Ltd kilichopo wilayani longido mkoani Arusha.

Ad

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea kiwanda hicho na kupokea changamoto kubwa kutoka kwa wawekezaji hao,kuwa wafugaji wengi bado wanapeleka mifugo yao nchi jirani ya kenya kwa madai ya bei kuwa juu kuliko hapa nchini.

Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo akiwa anajiridhisha na maelezo ya Mkurugenzi wa kiwanda hicho Shabbir Virjee katika Ziara ya Naibu Waziri kiwandani hapo Pauline Gekul.

Gekul alisema kuwa ni vema wafugaji wakawa wazalendo kwa kuuza mifugo yao kiwandani hapo, kwa kuwa uchakataji wa mazao hayo yanafanyika hapa nchini na faida nyingi zinakuwa kwaajili ya kunuafaisha taifa pamoja na kuingiza fedha za kigeni.

“Wafugaji ifike mahali sasa tuwe wazalendo kwa kuuza mifugo hapa nchini na ifike mahali tujisikie vibaya kunuifaisha watu wengine au Taifa lingine,Mifugo itoke Tanzania iende kunuafaisha Kenya,ichakatwe Kenya faida yote iende huko ndugu zangu hapa hatumuungi mkono, Maana kwa matendo haya kiwanda kinakosa malighafi.”alisema Gekul

Aidha alisema changamoto ya wingi wa tozo amelichukua na kuahidi kuwa wizara yake chini ya waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki watakahakikisha kuwa wanaketi na wizara ya fedha kuweza kutengeneza mazingira wezeshi na rafiki kwa wawekezaji hao.

Muonekano pichani Ni nyama ya mbuzi katika kiwanda Cha Eliya food Overseas Ltd, kilichopo wilayani longido zikiwa zimehifadhiwa kitaalamu kwaajili ya kusafirishwa nje ya nchi.

Na.Ashura Mohamed -Longido.

“Hili la Kodi nimelichukua tutakaa chini mapema sana na kuhakikisha tunatatua changamoto hii na niwaombe wafugaji kiwanda hiki kisikose Malighafi,tutakaa chini na waziri wa fedha na Kamati ya bajeti na kushauriana nao,ili mwekezaji huyu wa Elia Food Overseas Ltd atoe bei nzuri kwa wafugaji na wauze mazao hapa”alisema Gekul.

Naye mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe alisema kuwa kiwanda hicho Ni mkombozi kwa wafugaji wa mikoa ya Kaskazini na jirani hata kwa nchi kwa kuwa wafugaji wataweza kupata soko la uhakika na kuondokana na ufugaji wa mazao wa mifugo mingi ambayo haina tija.

“Mheshimiwa Naibu Waziri kwanza tunashukuru serikali kwa kuweza kuwekeza hapa,na kwanza tumepata soko la kisasa la kimataifa la Mifugo lakini leo hii tunashuhudia kiwanda hiki kwa kweli Ni uwekezaji mkubwa Sana ila Sasa  Serikali tunaomba  iboreshe mazingira ya kibiashara na kuwezesha kiwanda hiki kushindana na nchi kama Kenya, Ethiopia na nyingine katika uzalishaji kwa kuondoa tozo hizi ambazo ni kikwazo kikubwa Sana “alisema Mwaisumbe.

Pia Mkurugenzi wa kiwanda Cha Elia Food Overseas ltd Irthan Virjee alisema kuwa kiwanda hicho kimeanza uzalishaji  na Kuna uwezo wa kuchinja mbuzi 2000 kwa siku na ng’ombe 500.

Pia alisema wamejipanga kuhakikisha  kuwa wanafanya vizuri katika bara la Afrika kwa kuhakikisha kuwa wanasafirisha nyama kwa wingi zenye viwango na ubora wa kimataifa.

Dkt.Jumaa Mhina ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido alisema kuwa watumishi wa Serikali ya wilaya hiyo wamefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wawekezaji hao na kuhakikisha kuwa kiwanda hicho kinapatikana na wizara ilipokea jitihada hizo ambazo ni ukombozi mkubwa kwa wafugaji nchini.

“Tunaomba wizara  hii iendele kutulea tunataka kufanya mabadiliko makubwa kwenye soko na kuhakikisha kuwa nchi yetu inafanya vizuri kwa mazao haya ya  Mifugo haswa nyama,na kuweka nchi yetu katika ramani na kuhakikisha kuwa tunaitendea haki nchi yetu kwa wingi wa mifugo na usafirishaji wa nyama ambayo inazalishwa na kuchakatwa Tanzania.”alisema Jumaa.

Ziara ya siku moja ya  Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi wiliayani longido ni kutembelea kiwanda hicho kilichopo katika Kijiji cha Eurendeke na Soko la kimataifa la mifugo ambapo pia aliweza kuzungumza na Wafugaji.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

8 Maoni

  1. вызов такси по телефону https://zakaz-taxionline.ru/

  2. Портал о Ярославле – ваш гид по культурной жизни города. Здесь вы найдёте информацию о театрах, музеях, галереях и исторических достопримечательностях. Откройте для себя яркие события, фестивали и выставки, которые делают Ярославль культурной жемчужиной России.

  3. Karim Benzema https://karimbenzema.prostoprosport-ar.com is a French footballer who plays as a striker for the Saudi Arabian club Al-Ittihad. He played for the French national team, for which he played 97 matches and scored 37 goals. At the age of 17, he became one of the best reserve players, scoring three dozen goals per season.

  4. Cristiano Ronaldo https://cristiano-ronaldo.prostoprosport-ar.com is a Portuguese footballer, forward, captain of the Saudi Arabian club An-Nasr and the Portuguese national team. European Champion. Considered one of the best football players of all time. The best scorer in the history of football according to the IFFIS and fourth according to the RSSSF

  5. Ali al-Buleahi https://ali-al-bulaihi.prostoprosport-ar.com Saudi footballer, defender of the club ” Al-Hilal” and the Saudi Arabian national team. On May 15, 2018, Ali al-Buleakhi made his debut for the Saudi Arabian national team in a friendly game against the Greek team, coming on as a substitute midway through the second half.

  6. Romelu Menama Lukaku Bolingoli https://romelulukaku.prostoprosport-br.com Futebolista belga, atacante do clube ingles Chelsea e da selecao belga . Por emprestimo, ele joga pelo clube italiano Roma.

  7. Bernardo Silva https://bernardo-silva.prostoprosport-cz.org Portugalsky fotbalista, zaloznik. Narozen 10. srpna 1994 v Lisabonu. Silva je povazovan za jednoho z nejlepsich utocnych zalozniku na svete. Fotbalista je povestny svou vytrvalosti a vykonem.

  8. Luka Modric https://luka-modric.prostoprosport-cz.org je chorvatsky fotbalista, stredni zaloznik a kapitan spanelskeho tymu. klub Real Madrid, kapitan chorvatskeho narodniho tymu. Uznavan jako jeden z nejlepsich zalozniku nasi doby. Rytir Radu prince Branimira. Rekordman chorvatske reprezentace v poctu odehranych zapasu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *