NAIBU WAZIRI MWITA WAITARA AMETEMBELEA MGODI WA DHAHABU WA GEITA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara (katikati) akikagua shughuli za uchimbaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) mkoani Geita na kuridhishwa na utunzaji wa mazingira mgodini hapo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara ametembelea Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) pamoja na vituo vya uchenjuaji wa dhahabu mjini Geita.

Waitara ameonesha kuridhishwa na hatua za usimamizi wa mazingira na taka hatarishi zinazofuatwa mgodini hapo na kusema kuwa zinasaidia katika kutunza mazingira.

Ad
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara (katikati) akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wakati wa ziara ya kikazi mkoani Geita na kuridhishwa na uzingatiaji wa hifadhi ya mazingira.

“Huu ni mgodi unaozingatia miongozo ya Serikali katika suala zima la utunzaji wa mazingira nimeridhika, nimeona mpango wenu wa rehabilitation (kurudisha ardhi iliyoharibiwa na kupanda miti) kwa mujibu wa miongozo, alisema.

Aidha, wakati alipotembelea vituo viwili vya uchenjuaji wa dhahabu vilivyopo mjini Geita, Waitara aliwataka wadau hao kuzingatia sheria ya mazingira wakati wote bila kusubiri kutembelewa na viongozi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akikagua bwawa la tope sumu (TSF) alipokuwa katika ziara ya kutembelea shughuli za uchimbaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) mkoani Geita.

Alitahadhalisha kuhusu hewa inayotoka juu baada ya mchakato wa uchenjuaji na kuelekeza wataalamu wafanye uchunguzi kubaini ina madhara kiasi gani kwa mazingira, binadamu na wanyama.

“Hatuna uhakika na hewa inayotoka juu ina madhara gani maana hapa mpo karibu na makazi ya watu hivyo naelekeza NEMC (Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira) wafanye ziara za kushtukiza kubaini mapungufu,” alisema.

Naibu Waziri Waitara yupo katika ziara mkoani Geita kuelimisha umma kuhusu juhudi za Serikali katika kulinda hifadhi ya mazingira, kuhamasiaha usafi wa mazingira, upandaji miti pamoja na kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Hifadhi ya Mazingira ya mwaka 2004.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA RAIS WA JAMHURI YA KENYA DKT. WILLIAM SAMOEI RUTO, NAIROBI NCHINI KENYA

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.