DKT. NDUGULILE AIPA SIKU 90 SHIRIKA LA POSTA KUBORESHA UTENDAJI NA UFANISI WAKE

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) na Naibu Waziri wake, Mhandisi Kundo A. Mathew (wa kwanza kushoto) wakikagua moja ya kifurushi wakati wa ziara yake kwenye Shirika la Posta Tanzania, Dar es Salaam

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ameipa siku 90 Shirika la Posta Tanzania (TPC) kuboresha utendaji kazi na ufanisi katika kuhudumia wateja na wananchi kwa ujumla katika shughuli za kila siku za uendeshaji wa Shirika hilo

Dkt.Ndugulile ameyasema hayo kwa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakati wa ziara yake ya kutembelea Shirika hilo, Dar es Salaam ambapo aliambatana na Naibu Waziri wake, Mhandisi Kundo A. Mathew, Katibu Mkuu, Dkt. Zainab Chaula na Menejimenti ya Wizara hiyo kwa lengo la kufahamu utendaji kazi wa Shirika ili kuhakikisha kuwa linahudumia vema wananchi

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyenyoosha kidole) akihoji utendaji kazi wa skana ya kukagua usalama wa vifurushi na vipeto vinavyoingia na kutoka nchini katika ziara yake ya kutembelea Shirika la Posta Tanzania, Dar es Salaam

Ameongeza kuwa TPC ipitie mikataba yake ambayo haina maslahi kwa Shirika na isimamie vizuri rasilimali zake ikiwemo viwanja, ofisi na magari kwa kuwa rasilimali ni mtaji na mtaji sio fedha ili rasilimali hizo zitumike kuongeza mapato ya Shirika

Vile vile ameiagiza  Wizara yake kushirikiana na TPC kufanya mapitio ya sera na sheria ya posta ili ziweke kuendana na wakati kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akihoji jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Kanaali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo (aliyevaa miwani) wakati wa ziara ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) ya kutembelea Shirika hilo, Dar es salaam

Pia, amewakumbusha kuwa na mahusiano mazuri baina ya viongozi, wafanyakazi, menejimenti na wajumbe wa bodi katika mazingira ya mahali pa kazi ili kuboresha na kuongeza utendaji kazi wa Shirika

Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang’ombe akitoa maelezo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) kuhusu utendaji kazi wa kamera maalumu zinazofuatilia usalama wa ofisi za Posta, Dar es Salaam

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew amelipongeza TPC kwa kutengeneza Mfumo wa Taarifa wa Posta ambao unasimamia na kufuatilia uendeshaji wa Shirika; malipo na ukusanyaji wa mapato; na taarifa za watumishi

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula, ameueleza uongozi wa TPC kuwa Wizara itaendelea kushirikiana nao ili kufanikisha utendaji kazi wa Shirika katika kuhudumia wateja

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) akimsikiliza Ruben Komba (wa pili kushoto), Meneja wa TEHAMA wa Shirika la Posta Tanzania akiwasilisha mifumo ya TEHAMA iliyotengenezwa na Shirika hilo wakati wa ziara yake kwenye Shirika hilo.Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Fadya Zam (wa pili kulia), mwakilishi wa Meneja wa Mkoa wa Posta wa Dar es Salaam kuhusu utaratibu wa kutuma vifurushi nje ya nchi. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri, Mhandisi Kundo A. Mathew na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu, wote wa Wizara hiyo PICHA NAMBA 8 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang’ombe (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake kwenye Shirika hilo, Dar es Salaam. Katikati anayesikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo

Na Prisca Ulomi, WMTH

Mwenyekiti wa Bodi wa TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo na Posta Masta Mkuu wake, Hassan Mwang’ombe wamemshukuru Dkt. Ndugulile kwa ziara yake na kulitaka Shirika liboreshe utendaji kazi wake na wako tayari kufanyia kazi yaliyoelekezwa

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI YATOA BILIONI 3 KULIPA WATUMISHI WA AFYA WALIOSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19

Na WAMJW – Kibaha, PWANI.Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe Samia Suluhu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.