NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA MIRADI YA UZALISHAJIMALI YA WATU WENYE ULEMAVU

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na Ndg. Galus Buriani (aliyekaa wenye ulemavu) wakati wa ziara yake ya kutembelea vikundi vya watu wenye ulemavu ambavyo vinajihusisha za shughuli za uzalishajimali na kuona namna walivyonufaika na mikopo inayotolewa na serikali kupitia halmashauri 10% (Wanawake 4%, Vijana 4% na Watu wenye Ulemavu 2%).
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga (kulia)akimsikiliza Meneja Karakana ya Disabled Aid & General Engineering (DAGE), Ndg. Henry Chacha (katikati wenye ulemavu) wakati wa ziara yake ya kutembelea vikundi vya watu wenye ulemavu ambavyo vinajihusisha za shughuli za uzalishajimali kupitia uwezeshaji wa mikopo inayotolewa na serikali kupitia halmashauri.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kikundi cha watu wenye ulemavu cha Disabled Aid & General Engineering (DAGE) kinachojishughulisha na ufundi vyuma katika eneo la SIDO jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa kikundi cha watu wenye ulemavu cha Disabled Aid & General Engineering (DAGE) Bw. Patrick Mdachi.
Muonekano wa Baiskeli ya Matairi Matatu inayotengenezwa na kikundi cha watu wenye ulemavu cha Disabled Aid & General Engineering (DAGE) kilichopo SIDO, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) akimsikiliza Katibu wa Kikundi cha Disabled Living Art Group kinachojishughulisha na uzalishaji wa viatu vya Ngozi katika eneo la Machinga Complex alipotembea vikundi hivyo kuona namna walivyonufaika na mikopo inayotolewa na serikali kupita halmashauri 10% (Wanawake 4%, Vijana 4% na Watu wenye Ulemavu 2%).
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kushoto) akijaribu makobasi “Sandals” alipotembelea Kikundi cha Disabled Living Art Group kinachojishughulisha na uzalishaji wa viatu vya Ngozi katika eneo la Machinga Complex, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kushoto) akiwa ameongozana na wanakikundi cha Disabled Living Art Group kinachojishughulisha na uzalishaji wa viatu vya Ngozi katika eneo la Machinga Complex pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam alipofanya ziara katika eneo hilo ya kutembelea miradi ya Watu wenye Ulemavu.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *